The House of Favourite Newspapers

Rosa Ree Aeleza Alivyomtosa FID Q

0
Mwanamuziki anayekuja kwa kasi, Rosa Ree

MWANAMUZIKI chipukizi anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Bongo Fleva, Rosa Ree ameeleza jinsi alivyomtosa Fid Q kwenye kolabo ya ngoma ya rapa huyo iitwayo Fresh.

Akibonga na Mikito Nusunusu Rosa Ree alisema alipigiwa simu na Fid Q akimweleza nia yake ya kutaka kumshirikisha katika ngoma yake mpya, kitu kilichomfurahisha na kumtaka amtumie ‘beat’ ili asikilize na kuingiza kipande chake cha sauti.

Msanii wa Bongo, Fid Q

“Fid Q alinitumia beat nikaingiza verse yangu, nilipomaliza nilimwambia autaarifu uongozi wangu (management) juu ya kazi hiyo, ajabu baada ya kumwambia hivyo, sikuiona tena simu yake, siku chache baadaye nikasikia ngoma ipo mtaani,” alimaliza Rosa Ree.

Leave A Reply