ROSA REE AMEBANA AMEACHIA , UGUMU TUPA KULE

Rosa Ree ni mmoja wa mabinti wanaokuja kwa kasi kwenye muziki wa Hip Hop barani Afrika akitokea Bongo Flevani. 

 

Rosa Ree ni binti wa Kitanzania ambaye jina lake halisi ni Rosery Robert. Alianza kusikika mwaka 2015 aliposainiwa kwenye Lebo ya The Industry inayomilikiwa na prodyuza Nahreel wa Kundi la Navy Kenzo.

 

Tayari Rosa Ree ambaye ni mzaliwa wa Moshi, Kilimanjaro, mkononi ana ngoma kali kama One Time iliyomtambulisha kwenye gemu kisha zikafuata nyingine za Up In The Air, Way Up, Marathon, Dow, Asante Baba U.N.I.T.Y na nyinginezo. Rosa Ree anasema alianza muziki tangu utotoni na kitu ambacho kipo kwenye damu. Akiwa mtoto alipenda sana kuimba nyimbo za mastaa kama Faith Evans na P Didy kabla ya kujikita kanisani na kubobea kwenye mapambio.

Rose Ree aliyezaliwa Aprili 21, 1995, wakati anaanza gemu alijinasibu kama bonge moja la mgumu huku akibana mambo f’lani ya malovee kwa muda mrefu, lakini wenyewe wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya kikombe cha chai ya rangi hivyo kwa sasa anaonekana kuachia na ugumu wote tupa kule.

 

Wiki hii amewashtua mashabiki wake baada baada ya kutupia picha mitandaoni akiwa na mwanaume deep kwenye mahaba kama yote. Rosa Ree ameonesha mapenzi yake hadharani kwa mwanamuziki kutoka nchi jirani ya Kenya, Timmy Ti Dad. Kupitia Ijumaa ShowBiz kubwa kuliko zote, Rosa Ree anafunguka mengi kuhusiana na uhusiano wake huo mpya wa kimapenzi kama ifuatavyo;

 

Ijumaa: Mambo vipi Rosa Ree? Mbona kama umekuwa kimya kidogo hapo nyuma? Nini kinaendelea?

Rosa Ree: Hapana, sipo kimya ila siku zote mwanamuziki mzuri anafanya kazi zake zinaonekana kisha anatulia kwa muda kidogo kusikilizia kabla ya kuibuka na kitu cha maana au kizito.

 

Ijumaa: Siku za nyuma kidogo ulikuwa unaachia picha ambazo zilikuwa zinazua sana utata kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu zilikuwa zikikuacha sehemu kubwa ya mwili wako wazi, kwa nini ulikuwa unafanya hivyo?

Rose Ree: Ni kweli, lakini unajua mimi ni mwanamuziki, siangalii mtu anasema vipi ilimradi tu simtukani mtu wala kumkwaza.

 

Ijumaa: Vipi kuhusu wazazi hawakumaini kwa sababu zilikuwa picha za hatari?

Rose Ree: Tangu zamani wazazi wangu wanajua mavazi yangu yakoje, kwa hiyo hilo sidhani kama lina shida, lakini pamoja na hayo, wazazi wangu ndiyo mashabiki wangu wakubwa na wanajua wazi mimi ni mwanamuziki.

Ijumaa: Ukisikiliza baadhi ya nyimbo zako za nyuma, kuna maneno makali unarapu, hiyo nayo haikuleta taabu kwa wazazi wako wanaposikiliza?

Rosa Ree: Unajua ni hivi, wazazi wangu wako tofauti sana wanaheshimu kitu ambacho ninakifanya hivyo hakuna tatizo zaidi ya kunipa hongera tu!

 

Ijumaa: Mara nyingi umekuwa ukificha uhusiano wako wa kimapenzi kwa muda mrefu, lakini hivi karibuni naona umeamua kuweka wazi kila kitu. Nini kimetokea au imekuwaje?

Rosa Ree: Ni kweli kabisa sikuwa nimependa kuweka wazi mapema kwa sababu zangu. Lakini sasa hivi ni wakati wake…hahaha…

 

Ijumaa: Ila jamaa anaonekana siyo raia wa Bongo, kwa nini uliamua kuvuka boda na kwenda nje ya Bongo?

Rosa Ree: Unajua mapenzi ni majani, huota popote, ni kweli ni Mkenya ila kikubwa niliona pia ni mwanamuziki ambaye anaendana na mimi katika vitu vingi sana.

Ijumaa: Kwa hiyo wewe na yeye mmeungana, mnaimba pamoja?

 


Loading...

Toa comment