The House of Favourite Newspapers

Rosa Ree: Natamani TID awe Champion tena -Video

Msanii Rosa Ree akifanya mahojiano na +255 Global Radio leo katika mjengo wa Global Group, Sinza Mori jijini Dar.

HITMAKER wa Ngoma ya Champion akiwa amemshirikisha, Ruby, Rosa Ree ametembelea mjengoni Global Group, Sinza Mori jijini Dar na kusema kuwa anatamani sana siku moja mkongwe katika Bongo Fleva, TID arudi na kuwa Championi kwa mara nyingine.

 

Rosa Ree aliyasema hayo katika mahojiano na radio janja ya +255 Global Radio kupitia Kipindi cha Bongo 255 kuwa, aliona vipande vya video mtandaoni vikimuonesha TID akibishana na
mtu kisha kupigana.

“Niliona kwenye mitandaoni nikajisikia vibaya sana sana. Natamani nimuone TID yule wa Zeze kwani ni kaka yangu. Tangu nilipokuwa mdogo sana nilikuwa namuangalia kama mtu mmoja anayefanya vizuri kwenye gemu Afrika Mashariki. Natamani kumuona TID tena, kumuona akiwa Champion kama zamani.
Natamani sana hicho kitu,” alisema Rosa Ree.

Rosa Ree pia alielezea namna anavyomkubali Ruby na kumuweka kwenye ujio wake mpya wa Champion ambao una maana ya kutokukata tamaa katika maisha.
“Nampenda sana Ruby, naamini Afrika nzima hakuna anayeimba kama Ruby. Sijui nieleze vipi, ni mtu ambaye yuko real, ana upendo sana ndiyo maana hata ikawa ni rahisi kufanya naye kazi kwani alinikubali na mimi uwezo wangu.

“Mtakuwa mnasikia mengi kutoka kwangu na Ruby, tuna uwezo wa kufanya kazi pamoja kutokana na jamii kuona kama wasanii wa kike hawapo pamoja na mimi malengo yangu siku zote ni  kubadilisha hii kitu ambayo imejijenga hata kwenye akili ya wanawake.”

Kupata mahojiano kamili unaweza kutembelea Global TV Online kupitia Mtandao wa Youtube. Pia unaweza kusikiliza moja kwa moja Global Radio kwa kupakua APP ya 255 Global Radio katika Playstore kwenye simu yako ya mkononi.
Imeandaliwa: Andrew Carlos/GPL

Comments are closed.