The House of Favourite Newspapers

ROSE MUHANDO AIANGUKIA SERIKALI

Rose Muhando

BADO afya ya mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando ni tete ambapo ameiangukia serikali imsaidie ili aweze kurudishwa nchini.  

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, msemaji wa Rose ambaye kwa sasa amelazwa hospitalini nchini Kenya, Daudi Mashimo alisema, muimbaji huyo anaiomba serikali imsaidie ili aweze kurudishwa nchini na kupatiwa matibabu zaidi.

 

Aliendelea kusema, Rose anahitaji kurudi nchini na kuja kutibiwa huku ambako ni karibu pia na ndugu zake na kwamba Kenya alikwenda kufanya huduma ya uimbaji. “Kiukweli Rose anahitaji sana msaada wa serikali ili aweze kurudi nchini aje atibiwe huku; maana ndiyo nyumbani kule Kenya alikwenda kikazi tu, hivyo anaiomba sana serikali iingilie kati hilo kwani mpaka sasa amelazwa hospitali.

 

“Pamoja na serikali pia anawaomba Watanzania wamuombee ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida ili aweze kuwaburudisha kama zamani,” alisema Mashimo. Hivi karibuni Rose alikwenda nchini Kenya kwa ajili ya huduma lakini alipofika huko akiwa kanisani tayari kwa kuanza kuimba mapepo yalimlipuka na kuanza kuzungumza mengi huku akiwataja aliowaita ni wabaya wake.

 

Video yake akiwa anaombewa ilisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambayo pia ilimuonesha akiwa amedhoofu afya huku mikono na uso vikionekana kama vimebabuka kwa moto. Baada ya video hiyo kusambaa siku chache baadaye hali yake ilibadilika ambapo alipelekwa hospitali (ambayo imefanywa siri) na watu waliotajwa kuwa wenyeji wake ambako amelazwa hadi sasa.

Comments are closed.