The House of Favourite Newspapers

Rose Muhando.. Apata gonjwa…

2

Muhando (5)Brighton Masalu

MWIMBAJI nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando amepatwa na gonjwa la ajabu ambalo licha ya kumtesa kila siku, lakini vipimo katika hospitali anazokwenda mjini Dodoma, havioneshi kitu gani hasa anaumwa, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.

Muhando (2)Akizungumza na gazeti hili Jumapili iliyopita, wakati wa tamasha kubwa la amani lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Rose alisema mara nyingi mwili wake hukosa nguvu, hujisikia maumivu makali mithili ya vichomi huku akitokwa na vipele vinavyowasha kama upupu.

Muhando (4)“Naumwa sana, sasa ukichanganya na maneno ya watu, basi najikuta naumia mara mbili, nimezunguka hospitali mbalimbali, lakini hawaoni ugonjwa wa moja kwa moja, zaidi ya kupewa dawa za kutuliza maumivu tu, natokwa na vipele, vinawasha kweli, wakati mwingine ni kama ninachomwa sindano, vikikauka vinaacha alama nyeusi na kuharibu muonekano wa mwili wangu, yaani naumwa kweli, nahitaji tu maombi yenu, nitakufa jamani,” alisema mwimbaji huyo.

Muhando (1)Licha ya maumivu hayo ya mwili, pia mwimbaji huyo alisema kitu kingine kinachomuumiza ni maneno ya watu juu yake ambayo wakati mwingine hayana ukweli wowote kama kumsema juu ya magonjwa na vitendo ambavyo hana.

Kutokana na hali hiyo, Rose alisema amekuwa akitumia muda mwingi kukaa ndani ili kujiepusha na maumivu ya alichokiita ‘masimango ya walimwengu’ na anapotoka ni kwa ajili ya kwenda kanisani pekee.

2 Comments
  1. Mary Y Mbise says

    Rose usiogope mungu yu pamoja na wewe,pokea uponyaji ktk jina la yesu

  2. Kimwama says

    Laana ya ukahaba na kumdanganya mungu.

Leave A Reply