The House of Favourite Newspapers

ROSE NDAUKA ACHOMOA KUBANJUKA NA DJ OMMY

Picha inayohusiana
Rose Ndauka

MSANII wa filamu Bongo ambaye amepotea kwenye ‘media’ kwa kipindi kirefu, Rose Ndauka amefunguka juu ya tetesi zinazoenea mitandaoni kuhusu mahusiano yake na DJ Ommy Crazy baada ya picha zao kusambaa na watu kujiongeza kuwa wawili hao wanatoka. Akizungumza na Amani, Rose alisema hamna chochote kinachoendelea kati yake na DJ

Ommy zaidi ya kuwa marafiki wanaosapotiana katika kazi hivyo kwenda kwake kwenye bethidei yake hivi karibuni kulikozua maneno lilikuwa ni jambo la kawaida tu na si vinginevyo.“Sina mahusiano na huyo mtu, mimi nilienda kwenye bethidei yake kama rafiki yangu tu na hakuna kingine. Nashindwa kuelewa hivi vitu vinatoka wapi? Wanataka mtu asimsapoti rafiki wa kawaida?” alihoji Rose.

Stori:Shamuma Richard, Amani

Comments are closed.