ROSE NDAUKA AFUNGUKA UKIMYA WAKE

MUIGIZAJI mwenye mvuto Bongo Movies, Rose Ndauka amefungukia ukimya wake wa muda mrefu na kusema kuwa majukumu yameongezeka na ndiyo maana amepotea.
Akizingumza na Amani, Rose alisema kuwa mtoto wake sasa hivi anakua na anahitaji mahitaji muhimu kama elimu bora na vitu vingine vingi hivyo lazima aangalie upande mwingine wa kufanya kitu mbali na filamu ila maisha yazidi kusonga mbele.
“Unajua Naveen anakua, sasa nikisema nikalie kazi moja ni ngumu sana, sasa hivi nimefungua House Beuty kwa ajili ya kupamba wanawake na masuala mazima ya urembo, kazi hii inaniongezea kipato na huku nikiendelea mdogomdogo na filamu,” alisema Rose.
Stori: Imelda Mtema, Amani


Comments are closed.