Rose Ndauka: Wasanii Acheni utoto

MANENO kuntu! Mwanamama wa Bongo Movies, Rose Ndauka ameibuka na kusema kuwa, siku zote mtu akiacha utoto, mambo lazima yamnyookee.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Rose alifunguka kuwa mastaa wengi wanapokuwa akili hazijakomaa vizuri, hufanya mambo mengi ambayo siyo sahihi, lakini kuna wakati unafika akili inakomaa, lazima maisha yapige hatua.

 

“Unajua huko nyuma unaweza usijue kama kuna maisha yanatakiwa yasonge mbele, lakini kama hauko tayari kubadilika kiakili, basi huwezi kusonga mbele.

Mimi niliacha utoto na kukubali kuwa ni mama Naveen na kila kitu kikanyooka,” alisema Rose ambaye ni mama wa mtoto mmoja.

Stori: Imelda Mtema, Dar


Loading...

Toa comment