Rose: Sasa ni Wakati wa Ndoa

MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amesema hivi sasa ndiyo wakati sahihi kwa upande wake kuingia kwenye ndoa na kutulia.

 

Rose ambaye wiki moja iliyopita alivishwa pete ya uchumba na mwanaume aitwaye Afidh, ameiambia IJUMAA SHOWBIZ kuwa, kuna wakati mtu ukikimbilia kwenye ndoa kama muda hujafika, ni vigumu.

“Sasa ni wakati muafaka wa kuingia kwenye ndoa. Ninakwenda kufanya maisha, najua akili yangu imetulia na mimeshakua vya kutosha hivyo naamini ndoa yangu itadumu na nitakuwa mke bora,” alisema Rose ambaye huko nyuma alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Maliki Bandawe aliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye Naveen.

Toa comment