The House of Favourite Newspapers

Rostam Aziz Alivyosaidia Kuanzishwa NHIF

Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ameweka wazi kuwa uamuzi wa kuwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ni mpango ulioasisiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz.
Katika kitabu chake cha ‘My Life, My Purpose’ alichokizindua wiki iliyopita jijiji Dar es Salaam, Mkapa ameeleza alijifunza mpango huo wakati mfanyabiashara huyo alipokuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga alikouasisi mwaka 1996 kabla ya kutangazwa rasmi kuwa wa kitaifa.
“Njia nyingine ya moja kwa moja ya kuwasaidia masikini ni kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ambao umejitolea kuzipatia familia hizo bima za afya.
“Nilijifunza kuhusu mpango huu kutoka kwa Rostam Aziz, Mbunge na mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa waliofanikiwa.
“Mwaka 1996 alianzisha mpango wa bima ya afya kwa wananchi wake wa Jimbo la Igunga kwa kiwango kidogo cha fedha ya Sh 10,000 ambacho kilisaidia familia yenye watoto wanne kutumia bima hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima. Tuliamua kuutangaza mpango huu kitaifa,” ameeleza Mkapa katika kitabu chake hicho.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Comments are closed.