The House of Favourite Newspapers

ROTARY DAR MARATHON 2018 YAVUNJA REKODI IKIADHIMISHA MIAKA 10

Baadhi ya wanariadha wakishiriki katika mbio za kumi za Rotary Dar Marathon 2018 ambazo hufanyika kila mwaka jijini Dar es salaam. Zaidi ya watu 15,000 walijitokeza jana jijini Dar es Salaam kushiriki katika tukio la mwaka huu ambapo mbio hizo ziliadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.

Dar es Salaam. Mbio za Rotary Dar zimevunja rekodi ya kipekee mwaka huu huku zikiadhimisha miaka 10 tangu zianzishwe mwaka 2009.
Zaidi ya washiriki 15,000 wameshiriki mbio hizo ambazo zimehusisha mbio ndefu za kilomita 42.2, nusu ya mbio hizo kilomita 21.1 ikijumuisha pia waendesha baiskeli, kilomita 9 na 5 ambazo zimejumuisha matembezi ya familia.

Mwaka huu pia Mbio hizo za Rotary zimefanyika Bukoba na Karagwe ambapo zaidi ya watu 1,400 walikimbia na kufanya matembezi ya hisani.

Mshindi wa kwanza wa mbio za Rotary Dar Marathon 2018 wa kilomita 21.1 kwa upande wa wanawake Catherine Syokao (Raia wa Kenya) akimalizia mbio hizo katika eneo la The Green, Oysterbay jana jijini Dar es salaam. Mbio hizo za Rotary zinaadhimisha miaka 10 tangu kuanza kwake mwaka 2009.

Mbio za Rotary Dar, ambazo hutazamwa kuwa ndio mbio na tukio kubwa la aina yake hapa nchini zimekuwa na hamasa kubwa katika kalenda ya michezo na matukio ya kijamii. Mbizo hizo zilijumuisha makundi na rika tofauti tofauti na pia wanariadha wa kulipwa kutoka Kenya, Rwanda, Uganda na Malawi.

Tukio la mwaka huu kama ilivyo ada kwa miaka tisa iliyopita limedhaminiwa na kampuni mbalimbali ikiwemo

image.gif

epsi, Ashton Media, Toyota, ALAF, Minet, Zoom Tanzania, Resolution Insurance, Clouds Media Group, Azam, Plasco, Insignia, Knight Support, Ashers Industries, Exim Bank, KLM, CSI Construction na Soft Tech.

Tukio hilo lilianza rasmi majira ya asubuhi ya siku ya Jumapili kwa wanariadha mbalimbali wa mbio ndefu za kilomita 42.2 kuruhusiwa, zikifuatiwa na mbio fupi za kilomita 21.1 kwa wakimbiaji na waendesha baiskeli.

Mbio hizo ambazo ziliwaonyesha wanariadha na waendesha baiskeli mbalimbali wakitumia barabara ya mwambao wa bahari kuelekea maeneo ya katikati ya jiji, zilifanikiwa kupata washiriki wa kwanza kurudi katika eneo The Green, Oysterbay saa 2.30 asubuhi ambapo kwa ujumla mbio hizo zilitawaliwa na wanariadha wa kulipwa ambapo washindi wa kiume ni pamoja na Samson Ntandu(mtanzania) kwa mbio ndefu za kilomita 42.2 akifuatiwa na Peter Sule(Mtanzania) na nafasi ya tatu ilienda kwa Dushimukiza Thomas kutokea nchini Rwanda.

Washindi miongoni mwa wanariadha wa kike ni Sara Ramadhani kutokea Tanzania wa pili ni Dorcas Chesano(Raia wa Kenya) na mshindi wa tatu ni Doris Fisha kutokea Malawi.

Kwa upande wa Tanzania wanariadha walioshinda mbio ndefu ni Samson Ntandu kwa mwanaume na Sara Ramadhani kwa wanawake. Ambao wamepewa udhamini kwenda kuiwakilisha Tanzania katika Mbio za Beiruit mwaka huu, kupitia SBC Pepsi.

(Kutoka kulia kwenda kushoto) Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio za Rotary Dar, Catherinerose Barretto, Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt na Mkurugenzi Mkuu wa SBC Tanzania (Pepsi) Avinash Jha wakipeperusha bendera kufungua rasmi mbio za Rotary Dar kwa mwaka 2018, hafla iliyofanyika jana siku ya Nyerere katika viwanja vya The Green, Oysterbay jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, mshindi wa kilomita 42.2 kwa upande wa wanaume Samson Ntandu ameeleza namna ambavyo amejisikia fahari kwa kazi kubwa ambayo waandaji wameifanya, huku akiongeza kuwa, “Tukio hili lilikuwa la kipekee na ni jambo jema kuwa, miezi ya kujifua niliyojipangia kwa ajili ya mashindano haya, imenilipa kwa kushinda,”alisema.

Akikabidhi tuzo kwa mwaka huu, mlezi wa Mbio za Rotary Dar, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ametoa wito kwa Watanzania kufanya mazoezi na kuwa mstari wa mbele kushiriki mbio hizi ambazo hazipo tu kwa ajili ya kuboresha afya zetu katika maisha ya kila siku, lakini kupitia ushiriki wao na michango yao wameweza kwa kiwango kikubwa kuyasaidia makundi ya watu wasiojiweza.

Alizipongeza klabu za Rotary Dar es Salaam kwa kuendelea kuandaa Mbio za Rotary Dar na kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali yenye matokeo chanya kwa jamii.

Mlezi wa otary Dar Marathon, Al-Haj Hassan Mwinyi akigawa zawadi kwa washindi Mbalimbali.

Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt alishindwa kuzuia hisia zake kutokana na furaha aliyokuwa nayo kwa rekodi kubwa ya mwaka huu. “Nimefarijika sana kwa michango yenu ya kipekee ambayo imewezesha kuweka historia katika hitimisho la mwaka huu. Ninawashukuru watu wote ambao mmelifanya tukio hili kufana kuanzia wadhamini, waliojitolea, wana Rotary na kila mmoja wenu ambaye ameungana nasi. Haya yasingewezekana pasipo usaidizi wenu na kuamini jitihada zetu katika kufanikisha zoezi hili,”alisema Bi. Bhatt.

Aliendelea kuwakumbusha washiriki kuwa kila mmoja wao amekua msaada mkubwa katika kugusa watu wengi zaidi kupitia jitihada endelevu za ‘Rotary Dar Marathon’.

Mwenyekiti wa Mbio za Rotary Dar, Catherinerose Barretto alisema, “Tukio hilo ambalo lilianza tangu 2009 na washiriki 700 tu, kama wana Rotary tunajivunia kwa hiki tulichofanikisha kupitia misaada mkubwa kutoka kwa jamii na tutaendelea kujitolea zaidi kwa miaka mingi ijayo.
Washindi wengine katika mbio hizi ni Pamoja na:-

WANAUME KM 21.1
1 FARAJA LAZARO (TANZANIA)
2 DONALD MUSSA (KENYA)
3 JOSEPH PANGA (TANZANIA)
WANAWAKE KM 21.1
1 CATHERINE SYOKAO (KENYA)
2 NANCY JERAGAT (KENYA)
3 MARATHA YANKURINJE (RWANDA)
BAISKELI KM 21.1 (WANAUME
1 Mohamed Shamu (TANZANIA)
2 Musa Waer (TZ)
3 Hassan Amir (TZ)
BAISKELI KM 21.1 (WANAWAKE)
1 Hamida Ackland (TZ)
2 Upendo Nchome (TZ)
3 Tasmeen Hassan (TZ)

Comments are closed.