Kartra

RPC Adai Mbowe Alimwomba Luteni Urio Amtafutie Wanajeshi Wastaafu

MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama Kuu – Kanda ya Dar es Salaam, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Jumatano, Septemba 15, 2021 ambapo kesi hiyo inaendelea kwa shahidi namba 2, upande wa Jamhuri, RPC Ramadhan Kingai kutoa ushahidi wake.

 

Watuhumiwa wote wamesomewa mashtaka yao upya na kukana mashtaka hayo na kuendelea na mashahiti kutoa ushahidi wao.

 

Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Mustapha Siyai, Shahidi namba 2 upande wa jamhuri, Kamanda wa Polisi wa Kinondoni (RPC), Ramadhan Kingai amedai kuwa shahidi Na.1 Luteni Urio, aliombwa na Mbowe kumtafutia wanajeshi wastaafu ili kufanya vitendo vya ugaidi, miji ya Moshi, Arusha, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya.

 

Kamanda Kingai amedai pia kwamba Luteni Urio aliahidiwa kupewa cheo kikubwa jeshini baada ya uchaguzi mkuu kwa kuwa Mbowe atashika madaraka ya nchi.

Kesi bado inaendelea kusikilizwa…..


Toa comment