The House of Favourite Newspapers

RPC Kingai Kutoa Ushahidi Tena Kesi ya Mbowe Leo

0

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, leo Jumanne Oktoba 26, 2021 inatarajia kuendelea na kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ambapo Shahidi wa kwanza upande wa jamhuri, Ramadhani kingai ambaye na Kamanda wa Polisi Kinondoni DSM anatarajiwa kutoa ushahidi wake.

 

Kesi hii imekuja baada ya siku chache kupita tangu, Jaji Kiongozi Mustapha Siyani kutupilia mbali mapingamizi ya upande wa utetezi katika shauri dogo ndani ya kesi ya msingi juu ya maelezo ya mshtakiwa wa kwanza Adam Kasekwa ambapo upande wa utetezi ulitaka maelezo hayo yasipokelewe kama kielelezo cha ushahidi katika shauri hilo.

 

Mpaka sasa washtakiwa wamekwishafikishwa mahakani kwa ajili ya kuendelea na ushahidi mbele ya Jaji Mpya kutoka Mahakama Kuu Mwanza, Joachim Tiganga ambaye ameshika shauri hilo baada ya aliyekuwa akisikiliza shauri hilo kujitoa kutokana na kuongezewa majukumu mengine ya kiungozi.

Leave A Reply