The House of Favourite Newspapers

RPC Muruto Aanzisha Heka Heka Vijiwe vya Madada Poa, Tapeli Mbaroni – Video

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limeanzisha msako maalum uitwayo Oparesheni Heka Heka kwa Vijiwe vya Madada Poa yenye lengo la kutokomeza kabisa tabia ya baadhi ya mabinti na wanawake wanaofanya biashara haramu ya ngono kwa kuuza miili yao mkoani humo.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma leo Oktoba 9, 2018, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Girres Muroto amesema oparesheni hiyo imeanza Oktoba 3, mwaka huu na inalengo la kuwasaka wahalifu wote wa makosa mbalimbali mijini na vijijini ili kutokomeza vitendo hivyo mkoani humo.

 

Jeshi hilo limemkamata mtu mmoja anayeitwa Marobo Masanja mkazi wa Mpwapwa, akiwa na gobole lenye risasi 16, pamoja na risasi 47 zilizotengenezwa kienyeji, pia amekutwa na kilo 3.5 za bangi na kilo 5 za mbegu za bangi na mwingine akiwa na misokoto zaidi ya 300 ya bangi.

 

Aidha, Jeshi hilo limemkamata mtu mmoja akiwa na wenzake watatu akitokea Mbeya na alikuwa akijifanya kuwa ni askri wa Jeshi la polisi na kuwatapeli watu.

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.