The House of Favourite Newspapers

RUBANI AJITOSA KUMUOA WEMA!

UKISIKIA neno “Zali la Mentali 2019”, maana yake bahati ya mwaka iliyoje; sasa usiishie hapo ipeleke kwa staa wa filamu nchini, Wema Isaac Sepetu, halafu pumzika kidogo Ijumaa Wikienda likupe mchapo kamili.

Mwigizaji huyo kaangukiwa na zali gani? Habari za mjini zinasema kuna rubani mmoja wa ndege anayejulikana kwa jina la Ham­dan Zakwani ‘Danzak’ amejitosa kumuoa staa huyo ambaye ni Miss Tanzania 2006, kwa gharama yoyote.

 

RAFIKI WA RUBANI AFUNGUKA

Akizungumza na Ijumaa Wik­ienda, rafiki wa karibu na rubani huyo anayerusha ndege aina ya Dreamliner ya shirika moja la nchini Uarabuni (Hakupenda kutaja jina la shirika hilo) alisema kuwa, siku nyingi alikuwa na ndoto za kufunga ndoa na staa huyo lakini hakupata muda wa kufanya hivyo kwa kuwa, alikuwa amebanwa na masomo.

“Danzak alianza kumpenda Wema, kipindi kirefu sana na mara nyingi alikuwa akimfuatilia nyendo zake na kumpenda jinsi alivyo,” alisema rafiki huyo.

 

DANZAK ATUA NCHINI

Rafiki huyo aliendelea kuweka wazi kuwa, Danzak ametua hapa nchini kwa shughuli zake binafsi likiwemo suala la kuweka sawa mipango ya kumuoa Wema.

“Baada ya kumaliza masuala yake ya kimasomo na kuajiriwa, ameamua kuja nyumbani kupumzi­ka kidogo na mimi nimekuwa kama mwenyeji wake, kwa sababu za­mani kabla hajawa rubani tuliwahi kufanya naye sanaa ya muziki,” alisema rafiki huyo.

 

MSIKIE MWENYEWE DANZAK

Baada ya gazeti kuzungumza na rafiki huyo lilimpata Danzak mwenyewe ambapo aliamua kufunguka kuwa ni kweli kabisa anampenda Wema, tangu miaka ya nyuma na hajawahi kuacha kumpenda pamoja na mapito yake yote ya kimaisha.

“Nilitamani sana safari hii niliyokuja nionane naye, tukubal­iane mwanzo wa maisha yetu lakini nimekosa nafasi kutokana na mambo yalivyonibana.

“Hata hivyo kuna watu nimewaa­giza wafike nyumbani kwa akina Wema wakaeleze nia yangu, lakini wakiweza wamwambie Wema mwenyewe lengo langu kwake na thamani yake katika maisha yangu,” alisema Danzak.

Aliongeza kuwa, kutokana na majukumu ya kikazi yalivyo amelazimika kuondoka na kwamba atarudi miezi michache ijayo kuka­milisha mipango endapo ombi lake litakubaliwa.

 

WEMA ATAFUTWA

Gazeti hili lilimtafuta Wema ili aweze kuzungumzia zali alilolipata la kupendwa na rubani lakini haku­weza kupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kutopokelewa.

Hata hivyo, alipotafutwa katibu wake, Neema Ndepanya alisema yeye hajaambiwa kuhusu suala hilo lakini kama jambo hilo la heri lipo basi lifuate njia sahihi.

“Kama huyo rubani yuko ‘siriaz’ nyumbani kwa Wema hapapo­teleki, afike au hao aliowatuma waje, Wema watamuona na watazungum­za naye,” alisema Neema.

 

DANZAK NI NANI?

Danzak ni Mtanzania, ambaye kabla ya kwenda masomoni nje ya nchi amewahi kufanya kazi za muziki ka­tika Kundi la TNG Squard lililokuwa likiundwa na wasanii Agustino John ‘Latino Man’ na Malicki Bandawe.

Mbali na kurusha ndege im­eelezwa kuwa, rubani huyo shughuli za kimuziki bado ziko kwenye damu na kwamba hata alipofika Bongo kwa siku chache aliweza kutunga na kurekodi nyimbo mbili ambazo ni Fall In na Kichaa.

Endapo ndoa ya Wema na ru­bani huyo itafanikiwa, huo utakuwa mwanzo mwema wa maisha ya mwigizaji huyo mrembo ambaye hivi karibuni alikumbwa na tuhuma za kusambaza picha zisizokuwa na maadili, kosa ambalo limemfikisha mahakamani.

MCH WA AMBER RUTTY – “Natabiri Waziri Atakufa 2019”

Comments are closed.