The House of Favourite Newspapers

Rubani Gibuyi Hajaonekana Siku 15 Leo

0

MKUU wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amesema leo zimetimia siku 15 huku Rubani Samwel Gibuyi akiwa hajaonekana tangu aruke na ndege ya Shirika la PAMS Foundation wilayani Tunduru Oktoba 18, 2021 saa 9 bado wala ndege hiyo haijaonekana.

 

===============================

HATUJAMPATA

Leo ni siku ya 15 tangu Ndg. yetu Rubani Samweli Balina Gibuyi aruke na ndege ndogo aina ya BATAWK yenye nambari za usajili 5H – WXO mali ya PAMS FOUNDATION kutoka hapa Tunduru.

Rubani Samwel alitarajiwa kutua alitarajiwa kutua Kingupira (Selous) saa 11.30 jioni ya tarehe 18 Oktoba 2021 lakini hakutua na hadi leo hatujui alipo.

Kwa sasa (leo 02 Novemba 2021) vikosi vyetu vya ardhini vimeweka nguvu maeneo ya misitu na mapori yanayozunguka mto Mtetesi ambako tumekuwa tukipokea taarifa nyingi zenye ushawishi kuwa tufanye ukaguzi mkubwa kwenye eneo hilo.

Tuendelee kumwomba Mungu atende japo kidogo tu!

Julius S. Mtatiro,
DC Tunduru,
02 Novemba 2021.

 

Leave A Reply