CAPTAIN Mario Magonga, aliyekuwa rubani wa Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, amefariki katika ajali baada ya ndege aina ya helikopta (chopper) aliyokuwa akiiendesha kuanguka katika Ziwa Turkana katika wilaya ya Turkana.
Polisi wamesema leo, Magonga alifariki pamoja na raia wote wanne wa Marekani aliokuwa akiwasafirisha baada ya helikopta hiyo kuanza kuporomoka karibu na Lobolo katika mbuga ya wanyama ya Central Island National Park, saa mbili usiku.
Comments are closed.