Rubani wa Makamu wa Rais Afariki kwa Ajali ya Ndege

CAPTAIN Mario Magonga, aliyekuwa rubani wa Makamu wa Rais wa Kenya,  William Ruto,  amefariki katika ajali baada ya ndege aina ya helikopta  (chopper) aliyokuwa akiiendesha kuanguka katika Ziwa Turkana katika wilaya ya Turkana.

 

Polisi wamesema leo, Magonga alifariki pamoja na raia wote wanne wa Marekani aliokuwa akiwasafirisha baada ya helikopta hiyo kuanza kuporomoka karibu na Lobolo katika mbuga ya wanyama ya  Central Island National Park, saa mbili usiku.

 

“Chanzo cha ajali bado hakijajulikana na maelezo ya waliofariki yatatolewa baada ya ndugu zao kujulishwa,” taarifa ya polisi ilisema ikiongeza kuwa helikopta hiyo ni miongoni mwa mbili zilizotua eneo hilo kuleta watalii.

Loading...

Toa comment