The House of Favourite Newspapers

Rubby atimuliwa THT

0

rubyNa Musa Mateja

MREMBO aliyeingia kwa mbwembwe nyingi kwenye game la muziki Bongo, Helen George ‘Ruby’, hatimaye uongozi wa Tanzania House of Talent ‘THT’, umeshindwa kuendelea kuvumilia maovu yake na kulazimika kumtimua.

Chanzo cha kuaminika kilichopo ndani ya taasisi hiyo kilitutonya kuwa, kutimuliwa kwa binti huyo kumetokana na kukithiri kwa tabia za utovu wa nidhamu jambo ambalo alikuwa akionywa mara kwa mara na uongozi bila kubadilika.

“Ruby katimuliwa THT, chanzo ni utovu wa nidhamu anaouonesha. Hana shukurani, imefika wakati akifanyiwa ‘intaviu’ anakuwa mgumu kuonesha kuwa anatokea THT, anapata shoo nyingi lakini hana nidhamu ya pesa, kwa hiyo uongozi umeshindwa kumvumilia,” kilidai chanzo hicho.

Gazeti hili baada ya kupenyezewa udaku huo lilimtafuta Mkurugenzi Mkuu wa THT, Ruge Mutahaba ili azungumzie sakata hilo ambapo alijibu kwa kifupi kwamba ni kweli Ruby amesimamishwa na uongozi baada ya kushindwa kufuata taratibu na sheria za taasisi hiyo.

Leave A Reply