The House of Favourite Newspapers

Rubi kubwa Zaidi Kutoka Msumbiji Yauzwa New York kwa Rekodi

0

Rubi kubwa zaidi kuwahi kupigwa mnada imeuzwa New York kwa rekodi ya chini ya $35m (£28m).

Jiwe hilo lenye karati 55.22, liligunduliwa mwaka jana katika mgodi mmoja nchini Msumbiji.

Kabla ya kukatwa ilikuwa karati 101. Limeitwa “Estrela de Fura” kwa Kireno likimaanisha Nyota ya Fura. Jina hilo linarejelea kampuni iliyochimba jiwe hilo.

Rubi zilizopigwa rangi ya zaidi ya karati tano ni nadra sana. Sotheby’s, ambao walipiga mnada jiwe hilo, iliielezea kama kito cha “mara moja katika maisha”.

Mnada huo huo pia ulishuhudia jumla ya rekodi iliyopatikana kwa almasi ya waridi. Jiwe la karati 10.5 kutoka Botswana inayoelezewa kama jiwe la kupendeza la zambarau linauzwa kwa chini ya $35m.

TAARIFA JUU ya SABAYA KUPIGWA RISASI na KUFA, WAKILI WAKE AZUNGUMZA na GLOBAL TV…

Leave A Reply