Ruby akerwa na wakatisha tamaa

rubyMsanii mwenye sauti ya kuvutia aliyeliteka soko la muziki wa Bongo Fleva kwa sasa, Hellen George ‘Ruby’ ametoa dukuduku lake moyoni juu ya watu wanaopenda kuwakatisha tamaa wasanii au mtu yeyote yule ambaye yuko kwenye harakati za kutafuta maendeleo kuwa hawezi kuyafikia malengo yake.

Akiyazungumza hayo pasipo kung’ata maneno, Ruby amesema kwamba katika siku za kwanza kuanza muziki, alijitahidi kuwashirikisha baadhi ya watu mipango yake lakini kitu cha ajabu wengi walimkatisha tamaa na kumwambia hawezi kwani wengi walijaribu na mwisho wa siku walishindwa na kukaa chini ila alipoamua kufanya hivyohivyo, akafanikiwa kushinda.

“Sidhani kama Mungu aliumba watu wawe wanawakatisha tamaa wengine, hii ni tabia ambayo inakua kutokana na mtu anavyojiweka. Nilishawahi kukatishwa tamaa na kuambiwa kwamba sitaweza, ila mwisho wa siku nikaamini kwamba nitashinda, nikafanya na kweli nikashinda. Watu hawa wanawarudisha nyuma watu na kuwafanya kujiona kwamba hawawezi kabisa,” alisema Ruby.

 JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Loading...

Toa comment