The House of Favourite Newspapers

Ruck Baby: Nipo Tayari Kuolewa na Gadner

STORI: MAYASA MARIWATA | AMANI | SHOW BIZ – EXTRA

MWANADADA anayechipukia kwenye ulimwengu wa muziki Bongo, Rucky Baby ambaye ni mwandani wa mtangazaji maarufu Gadner Habashi amefunguka kuwa, mwanaume huyo kwa kipindi kirefu amekuwa akitaka amuoe akawa anamzungusha, ila sasa yupo tayari kuingia naye kwenye ndoa.

Gadner Habashi

Akibonga machache na paparazi wetu alisema ni ukweli usiopinga kuwa Gadner ni mtu wake na mapenzi yao huwa hayafi bali wanajipa likizo, jambo ambalo anashindwa kulipatia majibu kwa nini anashindwa kuachana mazima na mtangazaji huyo.

Rucky Baby

“Gadner ni mwanaume ambaye kuna kipindi tunaachana kila mtu anakuwa kivyake lakini tukikumbukana kama kawa, sababu mwenyewe huwa ananiambia hata nikiwa na mwanaume yeyote nikiona amenishinda nirudi kwake, kitambo tu aliniambia anioe nikawa nimepotezea hilo suala ili kuweka mambo yangu sawa, ila sasa naona bora anioe tu,”alisema.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.