The House of Favourite Newspapers

Rucky Baby, Mzaz Mwenziye Sasa ni Mapenzi Mubashara

 NA GLADNESS MALLYA | RISASI JUMAMOSI | MIKITO NUSUNUSU

BAADA ya hivi karibuni baba mtoto wake anayejulikana kwa jina la Kibabude kudaiwa kutoka kimapenzi na Wema Sepetu, msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Rukia Jumbe ‘Rucky Baby’ kwa sasa ni mapenzi mubashara na mzazi mwenziye huyo huku akieleza sababu za kuamua kuanikana mtandaoni.

Katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Kibabude aliweka picha ya Rucky Baby na kumsifi a kuwa ndiye mwanamke wa kwanza na pekee duniani huku mwanamama huyo akijibu hapohapo kwa kumsifi a baba mtoto wake huyo.

Akizungumza na Mikito Nusunusu , Rucky Baby alisema “Sisi mapenzi yetu yalikuwa ya kimyakimya hatukuwa na mbwembwe za kuanikana mitandaoni lakini maneno ya watu yalivyozidi mara Wema sijui nini ndiyo maana baba mtoto kaamua tuonyeshe mahaba hadharani ili kila mtu ajue,” alisema Rucky Baby.

Comments are closed.