The House of Favourite Newspapers

Rufaa Ya Pistorius Kusikilizwa Novemba 3 Mwaka Huu

0

PISTORIOUS (3)Oscar Pistorius akiwa mahakamani.PISTORIOUS (4)Baba mzazi wa aliyekuwa mpenzi wa Pistorious, Reeva Steenkamp, Barry Steenkamp akiambatana na mkewe, June wakati wa kusikiliza kesi ya mkwe wao.PISTORIOUS (2)Pistorius akiondoka Mahakama Kuu ya Afrika Kusini Oktoba mwaka jana baada ya kusikiliza kesi yake.PISTORIOUS (5)Pistorious and aliyekuwa mpenzi wake ReevaPISTORIOUS (1)Pistious (wa pili kulia) akiwa katika mashindano ya Paralympic, mbio za mita 100, London, mwaka 2012 

Johannesburg, Afrika Kusini

MAHAKAMA Kuu ya Rufaa nchini Afrika Kusini,  itasikiliza rufaa ya serikali dhidi ya mwanamichezo wa zamani mlemavu,  Oscar Pistorius, kuhusu hukumu dhidi yake Novemba 3 mwaka huu.

Tarehe 12 Septemba mwaka jana, Pistorious alifutiwa mashitaka ya kuua kwa kukusudia na badala yake akatiwa hatiani kwa kuhusika na kumpiga risasi na kumwua mpenzi wake wa kike aliyekuwa mwanamitindo na mwanasheria, Reeva Steenkamp, usiku wa kuamkia tarehe 14 Februari,  2013.

Pistorious alifyatua risasi nne  kwenye mlango wa maliwato uliokuwa umefungwa nyumbani kwake jijini Pretoria  Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) akifikiri ndani yake kulikuwa na mpita njia aliyeingia humo.

Tarehe 21 Oktoba, Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kumwua Steenkamp, na miaka mitatu ya kifungo cha nje kwa kuonyesha silaha hadharani katika mgahawa.

Mwezi ulipita Pistorius alikuwa aachiliwe kutokana na kuonyesha tabia njema gerezani, lakini katika dakika za mwisho Waziri wa Sheria na Misamaha ya Wafungwa, Michael Masutha, aliamua kusimamisha uamuzi huo.

Hii ni kutokana na barua iliyotoka kwa Umoja wa Harakati za Kupigania Haki za Wanawake wa Afrika Kusini iliyopingwa kuachiwa kwa Pistorius.

Leave A Reply