The House of Favourite Newspapers

Ruge Ajibu Kejeli za Mkuu wa Mkoa

0
Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

STORI: MWANDISHI WETU, UWAZI, HABARI

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, (pichani) amejibu kauli za kejeli zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa (RC) wa Dar Dar es Salaam ya kuwa yeye ni muongo na anafaa tu kuwa mwandishi wa mashairi na nyimbo za mapenzi na ngonjera.

Ruge ametoa kauli hiyo jana katika Kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo hicho, ambapo walikuwa na kipindi cha ‘Shukrani’ kwa wasikilizaji wao na watu waliowahi kuwasaidia kupata misaada. “Kila mtu ana mtazamo wake, na huwezi kulazimisha mtazamo wa mtu ubadilike. Inasikitisha sana kuona mtu anayesambaza haya mambo ni bosi wangu, bosi wa mkoa wetu. Yeye akipiga muhuri kitu ndiyo imekaa hiyo, yeye ana nguvu zote,” alisema Ruge.
“Sasa akisema hivyo mimi ni tapeli anataka kila mtu Dar es Salaam anione hivyo. Mimi sina nguvu kwa hiyo nachagua kubaki kwenye ninachokiamini. Tangu mwanzo nilisema mimi nataka haya mambo yaishe, cha kusikitisha huyu mtu ni kiongozi lakini anashindwa kumaliza jambo hili kwa busara na anataka kuliendeleza.

“Kuna mambo hapa najaribu kutengenezwa. Watu wanajaribu kutusukuma turudi kwenye mjadala ambao tulishaumaliza. Mimi ni mtu mzima na busara inaniambia watu wazima hatuna haja ya kurudi kwenye majibizano ambayo kwangu yaliisha siku nyingi,” alisema Ruge.

Hata hivyo, kipindi hicho kilikatizwa ghafla kwa sababu ambazo hazijajulikana. Mkuu wa Mkoa wa Dar jana alihojiwa ‘laivu’ na kituo kimoja cha televisheni ambapo baadhi ya maswali aliyoulizwa likiwemo la jina, hakujibu

Leave A Reply