The House of Favourite Newspapers

Rugemalira Acharuka Kortini, Atoa Notisi kwa Taasisi Tisa – Video

0

 

Mkurugenzi wa kampuni ya VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira amewasilisha notisi kwa taasisi tisa nchini Tanzania akitaka Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amuondoe kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili.

 

Ameeleza kuwa asipofanya hivyo atawasilisha rasmi hoja za kuondolewa katika kesi hiyo mahakamani.
Januari 30, 2020 mfanyabiashara huyo aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa ameandika barua kwenda kwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akielezea jinsi gani benki ya Standard Chartered ya Hong Kong walivyokuwa wakikwepa kodi na ushuru wa forodha.

 

Siku hiyo alidai Januari 24, 2020 aliongea na mwakilishi wa Takukuru alipotembelea gerezani na akamkabidhi nakala ya barua hiyo aliyoandika kwenda kwa Kamishna wa TRA lakini hadi sasa hajapata jibu lolote.

 

Pia, aliomba kesi hiyo ilitajwa tena, yaani leo upande wa mashtaka kuleta majibu kwa sababu wanaostahili kushtakiwa katika kesi inayomkabili ni benki hiyo.

 

Leo Alhamisi Februari 13, 2020 Rugemalira ametoa notisi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa. “Mheshimiwa hakimu nilitoa notisi sehemu mbalimbali ikiwemo kwa DPP na tayari imepokelewa, leo hii nilitegemea naachiwa kwa kuondolewa katika shauri hili,” amesema Rugemalira.

 

Miongoni mwa taasisi alizopeleka notisi ni ofisi ya DPP, DCI (mkurugenzi wa makosa ya jina), Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Mkurugenzi wa Takukuru, Gavana wa Benki Kuu, Kamishna TRA, wakili mkuu wa Serikali, DK Clement Mashamba na Kamishna wa Magereza.

 

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Rugemalira na mwenzake Harbinder Seth ni kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi, kutoa nyaraka za kughushi.
Pia wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh309 bilioni.

 

 

Leave A Reply