Breaking News: Rugemalira, Kigogo IPTL Wasomewa Mashtaka 6 Kisutu, Wasweka Rumande

Watuhumiwa wakifikishwa Mahakamani Kisutu.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewafikisha mahakamani, mmiliki kampuni ya PAP, Habirnder Seth Singh na mfanyabiashara James Rugemalira kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Jemes Rugemalira akiwa mahakamani

 

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumatatu, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola amesema, “Leo nawapa taarifa kuwa tunawafikisha mahakamani watuhumiwa wawili, kwa makosa ya kuhujumu uchumi na mengine yanayofanana na hayo.”

Harbinder Singh Sethi (aliyevaa kilemba) akiwa na Jemes Rugemalira (mwenye mvi), wakiwa Mahakamani Kisutu Dar es Salaam leo

 

Amesema kwa muda mrefu amekuwa akiulizwa kesi za Escrow na kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) zimeishia wapi, hivyo taasisi hiyo imechunguza shauri hilo kwa muda mrefu na kujiridhisha kwamba linaweza kufikishwa mahakamani.

 

“Kwa hatua ya awali wataenda Mahakama ya Kisutu, baada ya hapo kuna utaratibu wa kimahakama, watapelekwa mahakama maalumu kutokana na kiwango cha hujuma kilichofanyika na fedha zilizohusika,” amesema Mlowola.

Wakili Onesemo Mpinzile akizungumza na wanahabari.

 

Kwa mujibu wa wakili wa watuhumiwa hao, Onesemo Mpinzile ameeleza kuwa washtakiwa wamesomewa mashtaka sita likiwemo la uhujumu uchumi.

“Kwa misingi ya kisheria, washtakiwa wamenyimwa dhamana na kurudishwa rumande hadi Julai 3, mwaka huu, huku upelelezi ukiendelea.

Harbinder Singh Sethi (aliyevaa kilemba) akiwa na Jemes Rugemalila (mwenye Mvi), wakiwa Mahakamani Kisutu Dar es Salaam leo

“Mawakili tutakaa kuona namna gani tutawasilisha rufaa yetu kwa kuwa Mahakama ya Kisutu imesema haina mamla kisheria ya kutoa dhamana kwa washtakiwa hao,” alisema Mpinzile.

PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS | GLOBAL TV ONLINE

VIDEO: Rugemalira, Kigogo IPTL Walivyofikishwa Mahakamani

Nishushe Idd Mosi… Roma Atawaongoza Wakali Hawa Kuliamsha Dude, Dar Live

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment