Russia Yazishambulia, Kuzikamata Meli Tatu za Kivita za Ukraine

Russia imezikamata meli tatu za jeshi la maji la Ukraine jana (Jumapili) katika pwani ya Crimea iliyotwaliwa na Russia baada ya kuzishambulia na kuwajeruhi askari kadhaa, hali ambayo inatishia kuanzisha mgogoro mpya wa hatari baina ya nchi hizo.

 

Habari za kijasusi za shirika la usalama la taifa la Russia (FSB) zimesema mwanzoni mwa wiki iliyopita boti zake za ulinzi zilikamata meli za kijeshi za Ukraine katika (bahari) Black Sea na zikatumia silaha kuzidhibiti zisiondoke, kwani zilikuwa zimeingia eneo hilo bila kufuata taratibu na zilipuuza maonyo ya kuzitaka zisimame.

“Silaha zilitumika kuzisimamisha meli hizo za Ukraine,” ilisema taarifa ya  nakuongeza: “Matokeo yake meli tatu za Ukraine zilikamatwa katika eneo la maji la Russia katika Black Sea.”

FSB limesema wanajeshi watatu wamejeruhiwa na wanatibiwa na kwamba maisha yao hayako hatarini.

Uhusiano baina ya nchi hizo ni mbaya hasa baada ya Russia kuitwaa kwa nguvu eneo la Crimea na kuchochea waasi wanaoiunga mkono Russia mashariki mwa  Ukraine, jambo linaloweza kuzua mgogoro mkubwa kati ya nchi hizo mbili.

Ukraine imekanusha jambo hilo na kusema meli zake hazikufanya jambo lolote baya.  Imesema huo ni uchokozi wa Russia na kuitaka jumuia ya kimataifa kuiadhibu.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana kujadili mgogoro huo.

Toa comment