The House of Favourite Newspapers

Ruvu: Hasira za Simba, Tunawamalizia Yanga

0

BAADA ya kipigo cha mabao 3-0 walichokipata kutoka kwa Simba, juzi Alhamisi, uongozi wa kikosi cha Klabu ya Ruvu Shooting umetamba kuwa, sasa hasira zao zote wanazihamishia kwenye maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Yanga utakaopigwa Juni 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa.

 

Kipigo dhidi ya Simba, ni cha nne mfululizo kwa Ruvu Shooting na kinaifanya klabu hiyo izidi kuporomoka kutoka nafasi ya nne ambayo walikuwepo mwanzoni mwa msimu huu, mpaka nafasi ya 10 ya msimamo baada ya kujikusanyia pointi 37 katika michezo 30 waliyocheza mpaka sasa.

 

Katika mchezo wa raundi ya kwanza timu hizo zilipokutana Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliopigwa Desemba 6, mwaka jana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Mchezo wa Juni 17, pia utapigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.

Ofisa Habari wa Klabu ya Ruvu, Masau Bwire, amesema: “Tumesikitishwa na matokeo ya mchezo wetu uliopita dhidi ya Simba, kwa bahati mbaya kipigo hicho kimetufanya tupoteze mchezo wa nne mfululizo, hii ni baada ya kupoteza mbele ya Kagera Sugar, Tanzania Prisons na Mbeya City.

 

“Uongozi hatujafurahishwa na hali hii na sasa tumejipanga vizuri kumaliza makosa tuliyoya onyesha, na tutahakikisha tunaanza mapema maandalizi ya mchezo wetu ujao dhidi ya Yanga ambao ni lazima tuhaki kishe tunapata pointi tatu muhimu katika mchezo huo.

Stori: JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave A Reply