The House of Favourite Newspapers

Rwanda: Makanisa 714 na Msikiti Vyafungwa

 

KIGALI, RWANDA: Serikali imeyafunga makanisa 714 na msikiti mmoja kwa kukosa kutimiza masharti yaliyowekwa ya usafi,  usalama na makelele wakati wa maombi.

Afisa wa Serikali, Justus Kangwagye, amesema kutumia uhuru wa kuabudu hakufai kuingilia haki za watu wengine.

 

 

Taarifa zinasema baadhi ya makanisa yamekuwa yakifanya kazi kwa kutumia mahema na hayana maeneo ya kutosha ya kuegesha magari ya waumini huku baadhi ya waumini wakiegesha magari yao pembezoni mwa barabara na kusababisha misongamano ya magari.

 

Aidha, amesema baadhi ya makanisa hayo yalikuwa yakifanya kazi bila kuwasilisha upya maombi ya leseni na kwamba hawataruhusu yafunguliwe.

MPAKA HOME: MUME WA MAREHEMU RECHO HAULE ATOBOA SIRI NZITO

Comments are closed.