The House of Favourite Newspapers

Rwanda Yanunua Ndege Ya Kisasa Ya Airbus

rwanda-air-1

Ndege aina ya Airbus A300-200 iliyonunuliwa na Shirika la ndege la Rwanda, Rwandair.

rwanda-air-3

Ndege hiyo ikimwagiwa maji kama ishara ya kupokelewa.

rwanda-air-2

Viongozi mbalimbali wakiwa nje ya ndege hiyo.
rwanda-air-4

Muonekano wa  ndani wa ndege hiyo.

Safari ya kwanza ya ndege hiyo itakuwa kwenda Dubai

Muonekano wa nje wa ndege hiyo.

Shirika la ndege la Rwanda, Rwandair, limezidisha ushindani katika uchukuzi wa ndege Afrika Mashariki na Kati kwa kununua ndege aina ya Airbus A300-200.

Ndege hiyo itawezesha shirika hilo kufika masoko ya Ulaya na bara Asia.

Mkuu wa shirika la Rwandair John Mirenge amewaambia waandishi wa habari kuwa ndege hiyo yenye nafasi ya abiria 244 ndiyo ya kwanza katika ukanda huu na ina teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu.

“Ukiwa angani ndani ya ndege hii unaweza kupiga simu, kupata ujumbe wako wa simu, ujumbe wa barua pepe, ujumbe wa WhatsApp na mawasiliano mengine. Haya hayakuwepo katika ndege nyingine tulizo nazo,” amesema.

Ni ndege iliyotengenezwa nchini Ufaransa na kununuliwa kwa kitita cha dolla milioni 200 za Marekani.

Bw Mirenge, anasema safari za shirika la ndege la Rwandair zilikuwa zinajikita sana Afrika magharibi na kati na kwamba ndege hii sasa inakuja kuongeza uwezo wa kuvamia masoko ya Ulaya, Asia na kusini mwa Afrika.

Safari ya kwanza ya ndege hiyo inatarajiwa kufanyika wikendi ijayo tarehe 8 kuelekea mjini Dubai.

Shirika hilo sasa linalenga kusafirisha abiria laki 750 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017.

Comments are closed.