The House of Favourite Newspapers

Saa 94 kabla ya kifo cha mtikila

0

mtikila-new-siteElvan Stambuli
Ni vigumu kuamini! Mchungaji Christopher Mtikila aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Msolwa wilayani Bagamoyo, Pwani, Jumatano iliyopita alitembelea ofisi za gazeti hili, Bamaga Mwenge, Dar na kuzungumza na waandishi wetu.

Mtikila ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), alifika katika chumba chetu cha habari saa 94 kabla ya kifo chake baada ya kuombwa na mwandishi wa habari hii aje ili afafanue jambo.

mtikil.pngKabla ya kufika katika ofisi zetu, Mchungaji Mtikila alipogiwa simu na mwandishi wetu kuombwa ‘apointimenti’ ya kukutana naye nyumbani kwake, alikubali.
Hata hivyo, muda wa miadi ulipofika alipiga simu kwa mwandishi wetu na mambo yalikuwa hivi;
Mtikila: Haloo.

Mwandishi: Haloo mchungaji, nipo njiani nakuja.
Mtikila: Unakuja nyumbani?

Mwandishi: Ndiyo, nipo kwenye gari nitakuwa hapo dakika tano zijazo.
Mtikila: Ahh! Pole sana. Samahani bwana, mimi nina masuala fulani ofisi za ardhi mjini, wameniita ghafla ndiyo maana nimekupigia.

Mwandishi: Kwa hiyo hupo nyumbani?
Mtikila: Nipo lakini natoka kwenda huko, nakuomba kusitisha safari nitakuja ofisini kwako nikimalizana na watu wa ardhi.
Mwandishi: Sawa.

Baada ya mazungumzo hayo, saa tisa alasiri, siku hiyo ya Jumatano iliyopita, Mtikila alifika katika ofisi zetu na alipokutana na mwandishi wa habari hii alianza kwa kusema, “Saa ya ukombozi,” mwandishi akamjibu, “Ni sasa.”

Mwandishi huyo alimpeleka moja kwa moja kwa Mhariri Mtendaji wa Global, Richard Manyota ili kumtambulisha kabla ya kufanya naye mahojiano.

Akiwa katika meza ya Manyota, aliombwa awasalimie wanahabari lakini alikataa katakata akidai kwamba ana muda mfupi, akaomba kwa siku hiyo asifanye hivyo.
“Kwa kweli jamani leo nafasi sina ya kuzungumza na wanahabari, tutafanya hivyo siku nyingine. Leo nimekuja kuitikia wito tu,” alisema Mtikila.

Akiwa na Manyota, Mtikila alishangaa kuona ndani ya chumba hicho cha habari kuna magazeti mengi yanayozalishwa lakini la siasa ni moja tu ambalo ni Uwazi Mizengwe ya Uchaguzi linalotoka kila Ijumaa.

“Haya magazeti yenu yanasomwa na watu wengi sana. Andikeni siasa pia mkichanganya na hizo za mastaa,” alisema Mtikila.

Baadaye aliingizwa kwenye chumba cha mahojiano ambapo hata hivyo, hakuwa tayari kufanyiwa mahojiano maalum kwa siku hiyo akasema atapanga siku ya kufanya hivyo baada ya kujiandaa.

Alipotakiwa aseme neno kuhusu uchaguzi mkuu ujao, alisema:
“Napenda kusema jambo moja muhimu. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa ni mtu na mkwewe. Regina Lowassa ni mtoto wa kaka yake Jaji Lubuva hivyo Lowassa ni mkwe wake. Hili watu wanapaswa kujua.”

Hata hivyo, Mtikila alisema angerudi tena ofisini kwetu kesho yake ili apate mwandishi kwa ajili ya kwenda Bagamoyo ambako alidai kuna Mwarabu mmoja anatuhumiwa kuwadhulumu wananchi haki zao. Hakufafanua kwa madai kuwa mwandishi wetu atakwenda kusikia kutoka kwa wananchi madai yao, kesho yake hakufika licha ya kumsubiri kwa saa nyingi.

Hata hivyo, Jaji Lubuva alipoulizwa na mwandishi wetu kama madai hayo yana ukweli au la alisema, alisema ni kweli yeye na Regina Lowassa wanatoka sehemu moja, Kondoa mkoani Dodoma lakini akashindwa kukubali au kukanusha kuhusu taarifa hizo kama wana undugu.

Leave A Reply