The House of Favourite Newspapers

SAA TISA USIKU KITANDANI MWANGU

Hii ni kolamu ya Gazeti la Amani la Global Publishers ambalo linatoka kila Alhamisi. Lengo la kolamu huu ni kufikisha ujumbe wa kuelimisha juu ya jambo fulani kwa mwandishi kujifanya anazungumza na watu mbalimbali waliotangulia mbele za haki kwa njia ya ‘ndoto’.

 

 

Kimsingi mwadishi anatumia maneno ya kufikirika kwa kujifanya anaota. Anajifanya amekutana na watu waliofariki na wanamuuliza maswali juu ya yale yaliyopo duniani. Wanauliza maswali kutaka kujua kuna maendeleo yoyote yamefanyika tangu wao waondoke?

 

Kama yapo mwandishi anawajibu na kama hakuna anawaeleza kwa staili ya majibizano na mwisho wa siku elimu inawafikia wahusika wanaotakiwa kubadilisha mambo.

Mwisho wa siku mwishoni mwa kolamu, mwandishi anaeleza kabisa mahojiano hayo aliyokuwa anayafanya si halisi bali ni ndoto.

Usiposoma mwanzo hadi mwisho ni rahisi kuhoji kwamba marehemu anaongeaje au ushindwe kabisa kupata maana. Nawashauri wasomaji wetu wawe wanaisoma vizuri kolamu hii kwani mbali ya kuelimisha, ujumbe wake unafikishwa katika staili ya kuburudisha.

Mhariri Amani-Erick Evarist

Comments are closed.