The House of Favourite Newspapers

SAA YA UKUTANI HAIVALIWI MKONONI

OHH Anti Naa siku hizi hachambi sana kama zamani, komaaa! Aliyekwambia hii kolamu ya kuchamba nani? Hee heeeiyaaaaa! Waswahili wanakwambia raha ya nanga baharini, mtoni utatoka na tope! 

 

Shoga kuna vitu vingine vinakera kama muuza karanga wa kutembeza mitaani, hajali unaongea na mtu vitu vya siri au nini yeye anakuonjesha tu, ukimuuliza oohh swaga za ng’ombe azijuae mmasai, shuuuutuuuuu!

 

Leo shoga niko na nyie mnaojifanya mnaingia kwenye uhusiano mwezi tu umevuta jiko unaoa, unajua alipotoka? Unajua ana magonjwa gani ya kurithi na mengine ya kuamb-ukizwa? Haloooo eehhh! Dunia simama nijishukie miye! Hivi ni nani aliyewadanganya kuwa mke au mume bora anapatikana mitandaoni tena mitandao ya kijamii sijui Facebook, WhatsApp na Instagram? Shoga hii ni sawa na kuingia msalani bila kubisha hodi au kupanda daladala halafu unasahau kituo, upo?

 

Juzi kuna msomaji kama wewe alinitumia meseji na kuanza kulalamika; “ohh, Anti Naa naomba nisaidie hapa nilipo nimechanganyikiwa, nilikutana na mpenzi wangu Facebook miezi miwili iliyopita, alikuwa akiishi mkoani, mwanzoni aliniambia ni mwalimu wa chekechea nikamwambia aje Dar nitamtafutia huku lakini lengo langu lilikuwa pia kuishi naye kwa kuwa nilikuwa nimesha-mpenda.

 

“Niliishi naye kwa wiki moja tu, siku moja nime-enda kazini narudi majirani wana-nisha-ngaa, wana-sema kuwa mke wangu huyo amech-ukua kila kitu na kwamba amewa-ambia tuna-hama na mimi sitaki mtu ajue. Anti naomba msaada wako, mwanamke kanikomba kila kitu na sipajui hata anapoishi,” alisema msomaji huyo. Nikugeukie na wewe jamaa unayekariri kuwa maisha yote yanapatikana mitandaoni, hata kuchagua mke unataka mtandao ndiyo ukuchagulie, haya tena una bahati sana amekukomba kila kitu. Je, angekufanyia umafia ungekuwaje?

 

 Hatukatai kuwa ukitaka kujua kinyonga ana mbio kushinda swala choma msitu moto, lakini jamani kweli kabisa unamuamini mtu kwa asilimia zote kisa ulimuona mtandaoni, shuuuuutuuuu! Kwa taarifa yako tu, gogo halisukumwi kwa mkojo na ukitaka kujua nyama ina umaarufu huwezi kuikuta gengeni imechanganyika na mchicha pamoja na nyanya, heee heeeeiyaaaa! Unalooo shoga!

 

 

Tangu lini saa ya ukutani ikavaliwa mkononi? Labda nikung’ate tu sikio ung’atike shoga! Mwanaume au mwanamke wa kweli anampenda mtu anayemuona uso kwa uso, anamjua tabia zake kuanzia anapoishi hadi walezi wake, upo nyonyo? Kwa leo sitaki kuonekana muongeaji saana, naomba niishie hapa! Ni mimi Anti Naa Shangingi Mstaafu

Comments are closed.