The House of Favourite Newspapers

Sababu 5 za matajiri kuzidi kujituma licha ya mafanikio yao!

0

Katika maisha lipo suala la kufanikiwa lakini kwa waliofanikiwa si jambo la ajabu kusikia wamefilisika. Wapo ambao kipindi cha nyuma walikuwa na mafanikio makubwa lakini leo hii wamerudi kwenye umaskini.
Ndiyo maana kwa watu waliofanikiwa wasipokuwa makini ni rahisi sana kurudi kwenye umaskini endapo watashindwa kufuata kanuni zinazotakiwa.

Kutokana na uhalisia huo, tumekuwa tukishuhudia watu ambao wana mafanikio makubwa wakiendelea kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii. Utamkuta mtu ana mabilioni ya pesa benki, ana miradi kibao inayomuingizia fedha kila siku na mali nyingi lakini bado anapambana.

Hili utaliona kwa matajiri wakubwa duniani kama vile Warren Buffet, Bill Gates, Amancio Ortega, Carlos Slim na wale wa Tanzania kama vile Said Bakhresa, Raginald Mengi, Mohammed Dewji na wengine. Wana mafanikio makubwa lakini bado wanaumiza vichwa namna watakavyozidi kufanikiwa.

Unajua ni kwa nini? Sababu zifuatazo zinatajwa kuwasukuma matajiri wengi kuendelea kujituma usiku na mchana licha ya mafanikio makubwa waliyonayo;

Pesa zimewanogea
Mara nyingi ukishapata pesa, huwa zinakushawishi kuendelea kuzitafuta hivyo tajiri yeyote hujikuta akipenda sana pesa. Akishazoea pesa huwa hapendi kuona zinapungua. Zikipungua hujikuta anachanganyikiwa na kulazimika kufanya kazi kwa bidii ili ziongezeke na siyo kupungua.

Wanaogopa kurudi kwenye umaskini
Ukijaribu kufuatilia utagundua kuwa matajiri wengi duniani walianzia kwenye umaskini.
Waliogelea kwenye maisha ya kifukara kabla ya kucharuka na kutafuta pesa kwa nguvu zote. Walipofanikiwa hawakuwa tayari kuona wanarudi kule walikotoka.

Ndiyo maana matajiri wote duniani walio makini na maisha yao ni maadui wa wale wanaotaka kuwatibulia mafanikio yao. Pia wanajua kubweteka ni kujiweka katika mazingira ya kurudi kwenye umaskini, jambo ambalo hawataki kulisikia hata kidogo.

Wako kwenye ushindani
Watu waliofanikiwa wengi wao wanataka kuwa juu ya wenzao. Kwamba kama ni tajiri na anashika nafasi ya watano kwenye orodha ya watu matajiri kwenye nchi yake, atapambana ili siku moja ashike nafasi ya kwanza kama siyo ya pili. Mazingira hayo yanamfanya kila siku azidi kupambana akijua yuko kwenye ushindani kwani kuna uwezekano akicheza kidogo tu anatoka kwenye orodha ya watu matajiri, jambo litakalomkosesha amani ya moyo wake.

Wanaogopa aibu
Unajua ni kwa nini wengi wanapofilisika hujikuta wakijificha na kutotaka kuonekana kabisa? Hiyo ni kwa sababu wanaona aibu. Wanajua watakakokuwa wanapita watakuwa wakinyooshewa vidole na kusemwa vibaya, jambo ambalo linachukiza kupita maelezo.
Kwa maana hiyo kinachowafanya matajiri wengi wazidi kujituma ni kukwepa ile fedheha wanayoweza kuipata endapo watachezea maisha na siku moja wakafilisika.

Kujituma kuko kwenye damu
Asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa huenda ukiwauliza hobi yao kubwa nini watakuambia ni kufanya kazi kwa bidii. Hiyo ni kwa sababu imeshajengeka akilini mwao kwamba uvivu hauna nafasi kwa binadamu anayejua sababu ya kuletwa duniani.

Ndiyo maana unakuta matajiri wengine wenye makampuni yao wamejiwekea utaratibu wa kuwahi kazini kushinda hata wafanyakazi wao na wanafanya kazi hadi ‘over time’. Kwa nini? Kwa sababu kujituma kuko kwenye damu zao, kufanya kazi kwa bidii ni sehemu ya maisha yao ya kila siku. Ndiyo maana licha ya kwamba jamii inawaona wamefanikiwa

Leave A Reply