Sababu 5 Za Wasichana Warembo Kutoolewa

 

Wanawake wengi warembo/wazuri husalia peke yao na kufa katika hali hiyo kutokana na sababu tofauti.

Wengi huwa na tabia za kuudhi hali ambayo huwafukuza wanaume walio na uwezo wa kuwaoa.

 

Umewahi kushangaa sababu za wanawake warembo zaidi kutoolewa?

 

Umewahi kujiuliza Nani anataka kupanda miwa kwenye shamba karibu na shule?(sijui kama hiyo miwa itabaki salama na jopo lote la wanafunzi lililopo hapo shuleni)

 

Wanaume sio wajinga na katika asilimia kubwa ya wanawake wanaoolewa huwa ni waajabu sana ukiwaangalia kwa machoni kwa jinsi walivyo, mpaka unakuta wengine wanajiuliza,  ‘huyu mwanaume mzuri hivyo anamuoa mwanamke ambaye hawaendani’.

 

Ukiwa mzuri utapndwa na wanaume wengi ila watakupenda kwa lengo moja tu, ‘Mapenzi’ baada ya hapo utakuwa wa kuchezewa na kuachwa.

 

Kuna sababu tano ambazo huwafanya wanawake warembo/wazuri kusalia wapweke.

 

  1. Tabia

Wanawake kama hao huwa na tabia mbaya(uvaaji, ukaaji, viwanja vya starehe, lugha zisizo nzuri, marafiki) ambavyo hupelekea kuhatarisha nafasi yao ya kupata mume. Wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia za aina hiyo hata mwanamke awe mrembo kiasi gani.

 

  1. Baadhi ya wanawake hao huwa na maringo sana

Eti hawawezi kuosha nyumba kwa kuogopa kucha zao zisikatike. Wengine hawaju kupika na hawawezi kulea watoto kwa kuogopa kuchafuka.

 

  1. Ghali kuwatunza

Wanawake warembo huwa ghali kuwatunza kwa sababu huwa na dhana kuwa wanafaa kupelekwa katika hoteli kubwa kubwa na maeneo yaliyo na bidhaa ghali. Huwa hawalegezi msimamo hasa kuhusu mahitaji yao na wanakotaka kwenda kununua bidhaa.

 

  1. Wabinafsi na wenye chuki

Wanawake wa aina hiyo hufikiria dunia ni yao na kwamba wanafaa kuabudiwa na kila mwanamume. Wanaume wengi hupenda kuhusiana na wanawake wa aina hiyo, ambao huwadharau kutokana na kuwa “wanapendwa” na wanaume wengi.

Wasichojua ni kuwa wanaume huwatumia tu na kuwaacha kutokana na tabia zao ili kutafuta mwanamke mzuri wa kuoa.

 

  1. Hawataki kuwa wazazi

Wanawake hao hupenda kusalia wakiwa wa kupendeza, hivyo huwa wanaogopa kuzaa wasipate mikunjo, wasinenepe au kuwa na matiti kulegea. Kwa kawaida, hakuna mwanamume anayependa kuoa mwanamke ambaye hawezi kumzalia, hasa kwa sababu ya utamaduni wa Kiafrika.

 

Kama una sifa za aina hiyo, huenda ni wakati wako kubadilika ikiwa unataka kupata mume.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

 

Loading...

Toa comment