The House of Favourite Newspapers

Sababu 6 za wanaume kuwahi kufika kileleni -3

0

Kama tulivyoanza wiki iliyopita kuangalia tatizo hili la mwanaume kuwahi kufika kileleni na tuliangalia kuwa ni janga ambalo linawatesa wanaume wengi katika ulimwengu huu wa sasa kimyakimya.

Katika hili wanaume wamekuwa wakifanya jitihada binafsi kutafuta ufumbuzi ili kukwepa aibu kwa wenzi wao na kujishushia heshima.

Leo ningependa tuangalie tofauti ya mwanaume kuwahi kufika kileleni na kushindwa kutungisha ujauzito.

Kumekuwa na mitazamo mingi juu mambo haya kuna wanaodai ukiwahi kufika kileleni huwezi kutungisha ujauzito. Pia wapo wasemao kuwahi kufika kileleni siyo tatizo la kuzuia mimba kutungwa.

Kwa kuwa wiki iliyopita tuliangalia kwa kina tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni ni vema tukafahamu tatizo hili la kushindwa kutungisha ujauzito.

Tatizo la mwanaume kushindwa kumpa mimba mwanamke ni kubwa. Hii inatokea endapo wameishi pamoja kwa mwaka mmoja na tendo la ndoa likafanyika kikamilifu kwa lengo la kupata mimba lakini mimba hakuna. Hapa walengwa ni wanaume ambao wake zao wana afya bora ya uzazi yaani hawana matatizo yoyote katika mizunguko yao ya hedhi na hawana vimbe zozote katika via vyao vya uzazi. Kutokumpa mimba mwanamke kunasababishwa na ukosefu wa mbegu za kiume au kuwa na upungufu mkubwa wa mbegu za kiume. Tatizo huweza kumtokea mwanaume yeyote.

Tunaposema mbegu chache ni kwamba unapofikia kileleni wakati wa tendo la ndoa unatoa manii kawaida lakini ndani yake hakuna mbegu au mbegu zinakuwa chache, vilevile unaweza kutoa mbegu chache ambazo hazina ubora, tatizo hili kitaalam tunaita Oligospermia. Kuna wanaodhani mwenye mbegu chache ni yule anayewahi kufika kileleni ni kwa sababu ana mbegu za kiume chache ndiyo sababu ya kuwahi kufika kileleni.

Tunaposema mbegu ni chache kuliko kiwango ni kwamba unatoa kiwango cha mbegu za kiume chini ya milioni kumi na tano, kila tendo moja. Kiwango kikiwa chini ya hapo, basi uwezekano wa kumpa mwanamke mimba haupo na badala yake unafanya tu tendo la ndoa lakini uwezo wa kusababisha ujauzito haupo.

Usikose kufuatilia mada hii Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

Leave A Reply