The House of Favourite Newspapers

Sababu 6 za wanaume kuwahi kufika kileleni -4

0

couplesKama tulivyoona, wiki iliyopita tuliishia katika kuliangalia kwa undani tatizo hili la mwanaume kuwahi kufika kileleni kuwa ni kuhusu kuwa na mbegu chache za kiume.

unaposema mbegu ni chache kuliko kiwango ni kwamba unatoa kiwango cha mbegu za kiume chini ya milioni kumi na tano, kila tendo moja.

Kiwango hicho kikiwa chini ya hapo, basi uwezekano wa kumpa mwanamke mimba haupo na badala yake unafanya tu tendo la ndoa lakini uwezo wa kusababisha ujauzito haupo. Sasa endelea na mada yetu ili uweze kujifunza zaidi…

Pia kushindwa kutungisha ujauzito huambatana na mwanaume kuwa na idadi kubwa ya mbegu za kiume lakini hazina umbo stahiki yaani kichwa chenye umbo la yai na mkia mrefu unaoweza kuzisaidia mbegu hizo kupenya kwenye via vya uzazi vya mwanamke na hivyo kushindwa kutungisha ujauzito.

Dalili za upungufu wa mbegu za kiume
Mwanaume mwenye tatizo hili la kuwa na kiwango kidogo cha uzalishaji mbegu wakati mwingine hulalamika kukosa nguvu wakati wa tendo la ndoa, yaani unakuwa tayari lakini unashindwa kuendelea, hii ni kutokana na kuwa na upungufu katika mfumo wa homoni mwilini.

Maumivu na kuwepo na uvimbe kwenye korodani pia huchangia tatizo la uzalishaji wa mbegu za kiume kwa kiasi kikubwa.

Mwanaume ambaye haoti ndevu au vinyweleo mwilini pia hupata tatizo katika mfumo wa homoni hivyo hata uzalishaji wa mbegu za kiume nao huathirika.

Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume ambao unaweza kuwatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima. Kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu.
Usikose kufuatilia mada hii Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

Leave A Reply