The House of Favourite Newspapers

Sababu 6 za wanaume kuwahi kufika kileleni

1

MSOMAJI wangu karibu tena katika kona hii tupeane maarifa ya namna ya kuboresha afya zetu.

Wiki hii tutaanza kuangalia tatizo la wanaume kuwahi kufika kileleni au kuwahi kumaliza katika tendo la ndoa ikiambatana na uchovu wa ghafla wa kushindwa kurejea katika tendo na mbaya zaidi usingizi pia huwakumba ghafla wakiwaacha wenza wao bado na hisia kali za mapenzi.

Ninaliita hili kuwa ni janga la kitaifa kwa kuwa kliniki kwangu nimekuwa nikipokea wanaume wengi wenye tatizo hili lakini sababu ya pili ya kuliita janga la kitaifa ni kuwepo wanaume wengi wenye tatizo hili lakini hawajui kama ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine, lina vyanzo vyake na tiba kamili kwa hiyo wengi wao hubaki na tatizo hili likiwatafuna mpaka uzeeni.

VYANZO VYA TATIZO HILI;
Msongo wa mawazo
Wanaume wengi hasa wa mijini hujikuta katika msongo wa mawazo usiokwisha na hivyo hurudi nyumbani kutoka katika shughuli zao za kila siku wakiwa na hali hiyo.

Kujichua (masturbation) ni chanzo kikubwa cha tatizo hili kwa kuwa mara nyingi mvulana anapoanza mchezo huu huwa anafanya kwa siri na huhitaji amalize mapema kabla hajakutwa na watu na tabia hii hujijenga kisaikolojia na kujikuta mvulana/mwanaume huyu kuendelea na tatizo hili la kuwahi kumaliza hata katika tendo halisi.

Madhara haya ya kujichua huambatana na uume kusinyaa, kuwa mfupi na mwembamba tofauti na awali. Tafiti za kitabibu zinatabanaisha kwamba kila mwanaume aliyewahi kujichua mfululizo katika maisha yake ni lazima atakumbwa na tatizo hili kipindi fulani cha maisha yake.

Uoga/kutojiamini
Hali hii huwakumba wanaume wasio na taarifa kwamba wao ni wakamilifu, wanaume ambao hujidharau na kujiona hawafai kuwa na mwanamke wa hadhi fulani.

Kutofanya mazoezi
Inashangaza kuwaona watu wenye uzito mkubwa kupita kiasi au wazee au wagonjwa ndiyo wapo mazoezini asubuhi na jioni. Ila wanaume wengi hawana bidii ya kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.

Hali ya ulegelege hupunguza uwezo wa mwanaume kushiriki tendo la ndoa na ndiyo sababu mojawapo ya upungufu wa nguvu za kiume.
Usikose kufuatilia mada hii Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

1 Comment
  1. kulwa miraji says

    Mimi ninaswali hivi inakuwaje mwanaume hafiki kileleni nakama akifika anatoa mbegu ndogo mnooo kwanini?

Leave A Reply