The House of Favourite Newspapers

Sababu 8 Mourinho Amshukuru Van Gaal

jose-mourinho-louis-van-gaal-manchester-unitedMANCHESTER, England

MANCHESTER United imekuwa na kipindi cha miaka kadhaa ya mtikisiko tangu kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Alex Ferguson ambaye alistaafu.

Ujio wa makocha wengine klabuni hapo ilionekana hakuweza kusaidiz kurejesha heshima kubwa ya United katika soka la Ulaya na dunia kwa jumla kutokana na matokeo mabaya iliyokuwa ikiyapata.

Msimu uliopita timu hiyo ilikuwa chini ya Kocha Louis van Gaal, aliiwezesha kupata taji moja la FA lakini bado hakuwa kipenzi cha mshabiki wa timu hiyo kutokana na kutofanikiwa kupambana na vigogo wenzao kwenye soka la England na Ulaya kwa jumla.

Kocha huyo raia wa Uholanzi alikuwa na staili na mifumo yake ambayo haikuweza kufiboresha timu ndani ya muda mfupi, lakini sasa chini ya Kocha Jose Mourinho timu hiyo inaonekana kuanza kupata mwangaza mzuri wa kupata mafanikio.

Pamoja na hivyo bado kuna mambo mazuri ambayo yanafaida kutokana na uwepo wake klabuni hapo, na yawezekana Mourinho anafaidika kwa kuwa muda ambao Van Gaal alitumia kutengeneza mambo hayo, bado yalikuwa hayajakaa sawa.

Marcus-Rashford-648510MARCUS RASHFORD

Kijana ambaye ametokea kwenye chuo cha kukuzia vipaji cha United, hakuwa na nafasi kikosini lakini kutokana na kuonyesha uwezo wa juu katika mechi za vijana wenzake, alianza kupandishwa taratibu katika kikosi cha kwanza.

Van Gaal alianza kumpa nafasi hiyo mechi ya Europa dhidi ya FC Midtjylland baada ya Anthony Martial kuumia wakati akipasha misuli, Rashford atafunga mabao mawili na kuonyesha uwezo wa juu, huo ukawa mwanzo na sasa ni mmoja wa wachezaji wa kikosi cha kwanza licha ya kuwa ana umri wa miaka 19 tu.

Ameshathibitisha kuwa ni bora kutokana na kuzifunga timu kubwa zikiwemo Arsenal na Manchester City, Mourinho ameshamtabiria kuwa straika mkubwa siku za usoni.

337A500A00000578-0-Louis_van_Gaal_and_Anthony_Martial_are_joined_together_on_the_pi-a-5_1461446503656ANTHONY MARTIAL

Alipokuwa akisajili jina lake lilikuwa siyo kubwa Ulaya na duniani kote, ilitumika gharama kubwa kumsajili na wengi waliona kama Van Gaal amepoteza fedha nyingi kumsajili mchezaji ambaye hata straika wa United, Wayne Rooney alikuwa hamjui.

Akitokea Monaco mwaka 2015 wengi walitaka kuona uwezo wake uwanjani, akaanza kazi wa kuwavuruga Liverpool katika mechi yake ya kwanza tu.

Msimu wake wa kwanza alifunga mabao 17 katika mechi 49, msimu huu hakuanza vizuri lakini taratibu kasi yake imeanza kurejea na anaweza kufanya vizuri.

vangaalmourinhoUMILIKI MPIRA

United haikuwa timu ambayo inakawaida ya kumiliki mpira muda mwingi, yenyewe ilikuwa ikicheza mipira mirefu na kushambulia kwa kasi, lakini Van Gaal alianza kulibadilisha hilo na kutaka timu icheze pasi nyingi.

Ilikuwa ngumu mwanzoni na timu ilipoteza mechi nyingi kwa kuwa ilitaka kufanya kile ambacho kocha anakitaka.

Presha ilikuwa kubwa kwa kocha huyo ili timu ipate matokeo lakini yeye hakujali bali aliendelea kutaka wachezaji wake wacheze pasi nyingi. Licha ya kuwa alifukuzwa na nafasi yake kuchukuliwa na Mourinho, United imeendelea na staili yake ya kucheza soka la pasi wakati hiyo siyo falsafa ya Mourinho.

Mourinho anajulikana kwa kucheza soka la mbinu, kushambulia na kutotaka pasi nyingi lakini United ya sasa imo kwenye orodha ya timu zinazoongoza kwa kumiliki mpira.

ander-herreraANDER HERRERA KUWA MKABAJI

Aliposajiliwa United mwaka 2014 alikuwa ni kiungo mshambuliaji, Van Gaal hakufurahishwa na uwezo wake katika idara hiyo badala yake akaanza kupa majukumu mengine ambapo kwa sasa Mourinho anamtumia kama kiungo mkabaji.

Kutokana na kubadilishiwa majukumu mara kwa mara, Herrera sasa amefiti katika mbinu mpya za kuwa mkabaji akiwasaidia viungo wenzake.

daley_blind_of_manchesterDALEY BLIND KUMUDU NAFASI NYINGI

Alisajiliwa na Van Gaal, alikuwa akibadilishiwa majukumu mara kadhaa, kuanzia beki wa kushoto, kiungo mkabaji na beki wa kati kote alipamudu licha ya kufanya makosa kadhaa.

Chini ya Mourinho ameweza kufiti kuwa beki wa kati na mara kadhaa beki wa pembeni

antonio-valenciaANTONIO VALENCIA KUWA BEKI HALISI

Kuanzia enzi za Ferguson alitumika mara kadhaa kama beki wa kulia lakini Van Gaal alimtumia katika nafasi hiyo mara nyingi zaidi, kwa sasa Mourinho amemfanya kuwa beki halisi wa kulia wakati kiuhalisia alikuwa winga wa kulia.

marcos-rojoMARCOS ROJO KUWA BORA

Misimu yake mwili ya awali haikuwa mizuri, Van Gaal alimpa nafasi lakini bado hakuonyesha uwezo mkubwa wa kumshawishi, inavyoonekana alikuwa nazoea mazingira taratibu kwa kuwa kocha huyo ndiye aliyemsajili klabuni hapo.

Sasa chini ya Mourinho amekuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza na ameonyesha uwezo wa juu katika nafasi ya beki wa kati na hata anapopangwa pembeni pia.

KUWAIBUA CHIPUKIZI

Kawaida ya United inajulikana kwa kuwapa nafasi chipukizi wao, alifanya hivyo kwa wachezaji wengi akiwemo Timothy Fosu-Mensah.

Jesse Lingard na Rashford ni chipukizi wengine ambao walipata nafasi kubwa chini ya Van Gaal wakiwa bado hawajazoea mazingira, lakini Mourinho ameendelea kuwatumia kwa faida tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.

 

Comments are closed.