The House of Favourite Newspapers

Sababu Harmo, Kajala Kutohudhuria Kwa Barnaba Yawekwa Wazi… Soma Hapa

0
Msanii Harmonize au Konde Boy Mjeshi akiwa na na mchumba’ke, Kajala Masanja.

 

Labda unaweza kujiuliza ni kwa nini msanii Harmonize au Konde Boy Mjeshi hakuhudhuria kwenye tukio kubwa lililokusanya viongozi wakubwa wa Serikali, mastaa na watu kedekede kutoka ndani na nje ya Tanzania la uzinduzi wa albam ya msanii Barnaba Boy Classic iliyopewa jina la Love Sounds Different.

 

Katika tukio hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, mapema wiki hii, mashabiki walikuwa na shauku kubwa ya kumuona Harmonize na mchumba’ke, Kajala Masanja kama ambavyo walifanya mastaa wengine Bongo.

 

Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA umebaini kuwa hayo hayakuwa mapenzi ya Barnaba kutowaalika Harmonize na Kajala, bali mapenzi ya waandaaji wa shughuli hiyo ambao ni Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya Diamond Platnumz.

Inafahamika kwamba, WCB au Diamond na Harmonize hawana maelewano mazuri hivyo ingekuwa ni vigumu kuwaalika na hata kama wangewaalika, ingekuwa ni vigumu kwa wao kuhudhuria.

 

Hata hivyo, wachambuzi wanasema kuwa, waandaaji hao walijua kwamba, kama Harmonize na Kajala au kwa kifupi Harmojala wangehudhuria, basi wangeteka shughuli hiyo na wala Diamond na Zuchu wasingesikika kama ambavyo imetokea.

 

“Niamini mimi, Harmonize na Kajala wangekuja kwenye tukio hili ingekuwa ni balaa, kiki kubwa ingekuwa kwao na wala siyo Diamond na Zuchu kama ilivyotokea,” anasema Innocent Mawaya; mtangazaji wa vipindi vya mastaa kwenye Online TV na kungeza;

“Na kama ingetokea hivyo, basi watu wangeamini kwamba Harmonize amekua mkubwa kuliko Diamond.”

Stori; Sifael Paul, Ijumaa

MANARA AFUNGUKA – “NIMEKATAZWA HATA INSTAGRAM NISIPOST, WALA UWANJANI NISIENDE, NAHESHIMU ADHABU”

Leave A Reply