The House of Favourite Newspapers

SABABU KUBWA ZA WANAUME , WANAWAKE KUSALITI !

HAKUNA kitu kinauma kama usaliti. Usaliti ni jambo baya. Mwenzi wako anapokusaliti halafu ukagundua, kamwe huwezi kuwa na amani ya moyo. Akilini utajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu. Utawaza amekosa nini kwako, kwa nini akusaliti? Utaenda mbali zaidi; amekudharau? Hatambui thamani yako? Amekuona hufai? Haumtimizii mahitaji yake ya kifedha? Au haumtimizii mahitaji yake ya mwili? Ndugu zangu, usaliti janga baya. Ndiyo maana tumekuwa tukishuhudia hata mauaji kwa sababu ya usaliti. Mara nyingi anayesalitiwa hupata maumivu makali sana kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akimuamini mwenza wake.

Madhara yatokanayo na usaliti siku zote ni makubwa mno. Mtu anaweza kukusamehe mambo yote lakini usaliti huwa ni ngumu sana kuusamehe. Kovu la kusaliti huwa ni gumu kuondoka kwenye akili ya mwanadamu. Rinajirudiarudia kila wakati na linatesa nafsi. Unaposaliti na mwenzi wako akajua umemsaliti siku zote kuna mambo mawili; akusamehe na umhakikishie kwamba hutarudia, au akuache na kuanzia hapo uhusiano unakuwa umekufa jumla. Hili la kuachana jumla ndilo

ambalo watu wengi wame-kuwa wakilichagua. Ameku- fumania, hagombani na wewe wala aliyeku-fumania naye lakini biashara ndiyo inaishia hapo. Kama ni ndoa inakufa na kama ni uhusiano, kila mtu anachu-kua hamsini zake. Ni nadra sana kusikia mtu amfu-manie ampe-ndaye halafu ukaona penzi lao lime-rejea na limesi-mama kama zamani. Ndiyo maana leo nimeona tuziangalie baadhi ya sababu ambazo zinasa-babisha watu wengi wajikute wamesaliti.

MAZOEA

Suala la mazoea lina uwanja mpana kidogo. Kuna mazoea ya upande wa wahusika, yaani mke anamzoea mume kiasi cha kumuona kama vile kaka yake. Anajisahau kufanya majukumu yake

Comments are closed.