Sababu Mbili Zilizombakisha Saido Dar

IMEELEZWA kuwa sababu mbili kuu ndiyo zilizosababisha kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Said Ntibanzokiza ‘Saido’ kubakishwa mkoani Dar es Salaam.


Mrundi huyo alibakishwa
Dar katika msafara wa wachezaji 24 waliosafiri kwenda Songea kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC juzi Jumanne.

 

Kiungo huyo tangu kuanza kwa msimu ameonekana kutokuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Kocha Mkuu raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi.


Kwa mujibu wa taarifa
ambazo imezipata Championi Jumatano, sababu ya kwanza iliyosababisha kiungo huyo
abakie Dar kutokana na
kuchelewa kujiunga na kikosi hicho akiwa nyumbani kwao katika majukumu ya timu ya taifa.

Mtoa taarifa huyo alisema sababu nyingine ya pili ni kutokuwa fiti kwa asilimia mia moja zaidi ya nyota
waliosafiri nao kwenda
Songea kucheza mchezo huo.


“Saido ni kati ya wachezaji
waliobaki jijini Dar na sababu kubwa iliyomfanya abakishwe ni kutokuwa fiti.“Wachezaji wengine waliobaki Dar Balama (Mapinduzi), Ambundo (Dickson) na Yassin (Mustafa) ambao hao wote ni majeruhi wameanza mazoezi mepesi ya binafsi.


“Saido hana tatizo lolote
na timu, kwani hivi karibuni kuliibuka maneno mengi kuhusiana na yeye na kocha, timu itakaporejea ataungana na wachezaji wenzake mazoezini,” alisema mtoa taarifa huyo.


Alipotafutwa Meneja Mkuu
wa timu hiyo, Hafidh Saleh kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Kuhusu walioachwa wote ni majeruhi isipokuwa Saido aliyeshindwa kufanya mazoezi ya mwisho pamoja na timu baada ya kuchelewa
kuiunga na timu.


“Ngumu kwa kocha
kwenda na mchezaji ambaye ameshindwa kuwa pamoja na timu, hivyo amebakia Dar na atajiunga na timu baada ya kutoka Songea kucheza dhidi ya KMC.”2176
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment