SABABU WANAWAKE WAZURI KUTOOLEWA ZAANIKWA

WANAWAKE wengi warembo au wazuri husalia peke yao na kufa katika hali hiyo kutokana na sababu mbalimbali, Risasi Mchanganyiko limedokezwa. 

 

Akizungumza na mwandishi wetu, Mtaalam wa Saikolojia ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Chris Mauki alisema kuwa, wengi huwa na tabia za kuudhi hali ambayo huwafukuza wanaume walio na uwezo wa kuwaoa.

 

“Umewahi kushangaa sababu za wanawake warembo zaidi kutoolewa? Umewahi kujiuliza nani anataka kupanda miwa kwenye shamba karibu na shule?

 

(sijui kama hiyo miwa itabaki salama na jopo lote la wanafunzi lililopo shuleni hapo). “Wanaume siyo wajinga na katika asilimia kubwa ya wanawake wanaoolewa huwa ni waajabu sana ukiwaangalia kwa machoni kwa jinsi walivyo, mpaka unakuta wengine wanajiuliza; ‘huyu mwanaume mzuri hivyo anamuoa mwanamke ambaye hawaendani’.

 

“Ukiwa mzuri utapendwa na wanaume wengi ila watakupenda kwa lengo moja tu, ‘mapenzi’ baada ya hapo utakuwa wa kuchezewa na kuachwa. “Kuna sababu tano ambazo huwafanya wanawake wazuri kusalia wapweke kama ifuatavyo;

TABIA

“Wanawake kama hao huwa na tabia mbaya (uvaaji, ukaaji, viwanja vya starehe, lugha zisizo nzuri, marafiki) ambavyo husababisha kuhatarisha nafasi yao ya kupata mume. Wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia za aina hiyo hata mwanamke awe mrembo kiasi gani.

 

“Baadhi ya wanawake hao huwa na maringo sana. Eti hawawezi kuosha vyombo, kufanya usafi wa nyumba au kufua kwa kuogopa kucha zao zisikatike. Wengine hawajui kupika na hawawezi kulea watoto kwa kuogopa kuchafuka.

 

GHALI KUWATUNZA

“Wanawake warembo huwa ghali kuwatunza kwa sababu huwa na dhana kuwa wanafaa kupelekwa katika hoteli kubwakubwa na maeneo yaliyo na bidhaa ghali. Huwa hawalegezi msimamo hasa kuhusu mahitaji yao na wanakotaka kwenda kununua bidhaa.

WABINAFSI NA WENYE CHUKI

“Wanawake wa aina hiyo hufikiria dunia ni yao na kwamba wanafaa kuabudiwa na kila mwanaume. Wanaume wengi hupenda kuhusiana na wanawake wa aina hiyo, ambao huwadharau kutokana na kuwa wanapendwa na wanaume wengi. “Wasichojua ni kuwa wanaume huwatumia tu na kuwaacha kutokana na tabia zao ili kutafuta mwanamke mzuri wa kuoa.

 

HAWATAKI KUWA WAZAZI

“Wanawake wazuri hupenda kusalia wakiwa wa kupendeza, hivyo huwa wanaogopa kuzaa wasipate mikunjo, wasinenepe au matiti kulegea. Kwa kawaida, hakuna mwanaume anayependa kuoa mwanamke ambaye hawezi kumzalia, hasa kwa sababu ya utamaduni wa Kiafrika. “Kama una sifa za aina hiyo, huenda ni wakati wako kubadilika ikiwa unataka kupata mume,” alisema Dk Mauki.


Loading...

Toa comment