SABABU YA MAAMBUKIZI (INFECTION) YA SIKIO KWA WATOTO

MAAMBUKIZI au Infection ya masikio ni tatizo kubwa kwa watoto, sikio limejigawa sehemu kuu tatu ya ndani, nje na kati.  Matatizo mara nyingi yanashambulia sehemu ya kati ya sikio (Otitis media) inashambulia watoto wachanga na watoto wadogo na nyingine ni sehemu ya ndani ya sikio (Otitis externa).

Hii inawashambulia sana wale wanaoogelea mara kwa mara na pia linajitokeza kipindi cha baridi. Inakuwa ngumu mzazi kujua chanzo chake, kuna baadhi ya wazazi wanadharau kufuatilia tiba yake, mwishowe masikio ya mtoto hutoa usaha mzito na harufu kali na kumpelekea kuwa na tatizo la kutokusikia vizuri.

Hili tatizo linawashambulia sana watoto walio chini ya mwaka mmoja kwa asilimia 50, watoto walio na miaka mitatu na kuendelea kwa 70 na kwa watu wazima ni kwa asilimia 30. Husababishwa na bakteria au virusi wanaoshambulia kwenye ngoma ya sikio (ear drum).

Kuna sababu tofauti zinazochangia mtoto kupata infection ya sikio baada ya bakteria kushambulia kwa wazazi wanaovuta sigara na wanachochea kwa asilimia 37 ya kushambuliwa na infection ya sikio kwa urahisi.

MZIO (allergies)

Mtoto anapopata mzio au allergy unaweza kwenda kuziba mirija inayoungana na pua, koo na sikio la kati. Kufungwa kwa mirija husababisha kutengeneza majimaji masikioni yanayokuja kumletea maambukizi. Upungufu wa kinga mwilini unachangia mtoto kupata maambukizi pia.

Dalili ya mtoto mwenye maambukizi kwenye sikio ni mtoto kupata homa, kukosa hamu ya kula, kuhara na kutapika kwa wingi. Dalili nyingine ni kukosa raha na kulia sana kutokana na maumivu makali, kusugua au kuvutavuta sikio lake, sikio kutoa usaha wa njano au mweupe wenye harufu kali, kushindwa kulala, kuvimba sikio na macho kuwa mekundu na kushindwa kusikia vizuri.

Adhari ya kupata maambukizi (infection) ya masikio ni mtoto anatakiwa kupata tiba kwa haraka akiwa amepata maambukizi ya masikio sababu inamletea madhara makubwa kama ya kuweza kuwa kiziwi (mtoto anashindwa kusikia vizuri), kuugua uti wa mgongo, yaani mtoto anapata tatizo la uti wa mgongo baada ya bakteria kushambulia utandu (membrane) inayofunika ubongo na uti wa mgongo.

Madhara mengine ni kushambuliwa kwa ngoma ya sikio na baya zaidi ni mtoto kuchelewa kuongea.

TIBA YAKE

Uonapo dalili hizo, mpeleke mtoto haraka hospitali hasa kama ataanza kuharisha na kutapika! Dawa za kuua vijidudu au bakteria (Antibiotics) atapewa mtoto, ingawa kwa watoto walio chini ya miezi sita haishauriwi kupewa antibiotics kwani kuna dawa zao nyingine iwapo haikumtibu.

Kabla ya tiba mtoto atapimwa kama anaweza kusikia vizuri na wataalamu watatumia kifaa cha Otoscope -kinachoingizwa sikioni au mtoto atachukuliwa kipimo cha CT SCAN. Watoto wengine wanaweza kupatwa na infection ya sikio zaidi ya mara moja kinachotakiwa mzazi umpe dozi yote aliyoandikiwa na daktari.

USHAURI MUHIMU

Epuka kabisa tabia ya kumchokonoa mtoto sikio unapoona analia na kulishikashika. Tabia ya kumchokonoa mtoto imeshasababisha watoto wengine kupasuliwa ngoma zao za sikio na kutosikia kabisa.

Wataalamu wanashauri juu ya kusafisha masikio yako na vitu vya chuma, kama vile pini, loops, kwa sababu ya hatari ya kuumia. Aidha, vitu hivi vinaweza kusababisha kuvimba, kuumia kwa ngoma ya sikio (eardrum) na usafi usiofaa na mbaya.

Ikiwa una haja kubwa ya kusafisha masikio, basi unapaswa kuosha kwa kitambaa cha pamba kilichohifadhiwa na maji.


Loading...

Toa comment