Sababu za Utokwaji wa Majimaji Katika Via vya Uzazi vya Mwanamke

TABIBU WA AMANI| GAZETI LA AMANI| AFYA

Uhali gani mpendwa msomaji na mfuatiliaji wa makala hizi za afya. Leo tutakuwa na mwendelezo wa mada tuliyoianza wiki iliyopita.

Wiki iliyopita tuliangalia tatizo la utokaji wa majimaji katika via vya uzazi vya wanawake. Tuliona kuwa ni kawaida via vya uzazi vya wanawake kutoa majimaji lakini kuna majimaji ambayo ni kiashiria cha mashambulizi katika via vya uzazi. Na tuliona majimaji hayo huambatana na harufu mbaya, miwasho na huwa na rangi kama usaha. Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha mwanamke akakumbwa na tatizo hili kama vile:-

(i) Maambukizo / mashambulio katika njia ya uzazi ya mwanamke na si njia ya mkojo. Hii hutokana na kufanya mapenzi yasiyo salama na mtu ambaye ana magonjwa ya zinaa, na hivyo bakteria au virus au fangasi wanaoshambulia njia ya uzazi. Maambukizi haya yapo ya aina kubwa tatu ambayo kitaalam ni bacterial Vaginosis, Trchomoniasis na Monilia.

(ii) Kushiriki tendo la ndoa kinyume na maumbile na wakati huo huo kuhamia kwenye uke na kuhamisha uchafu na wadudu ambao hushambulia njia ya uzazi.

(iii) Ulaji mbovu . Utokwaji wa uchafu ni tatizo linalowakumba wanawake wengi wa mijini kwa sababu hii. Chakula kilichojaa mafuta kinachochea/kinaamsha seli za mafuta (fat cells) mwili mzima na hivyo husababisha kuzalishwa kwa homoni nyingi za ‘estrogen’. Homoni hizi zikiambatana na upungufu wa `fiber` zinachochea ukuaji wa bakteria wa ndani ya utumbo ambao kitaalam wanaitwa `Clostridia` ambao wanasifa ya kubadilisha `bile acid` kuwa homoni za ‘estrogen’ ambazo zinapozidi sana husababisha tatizo la mwanamke kutokwa na uchafu katika via vyake vya uzazi

(iv) Njia za kisasa za uzazi wa mpango (hasa vidonge) bila kujali ushauri wa mtaalamu na bila kujali usafi. Hivi huharibu ukuta wa uke (mucus membranes of the vagina) ambao ni ulinzi, hivyo huharibu afya ya uke kwani huufanya uwe na hali ya ‘alkali` hali ambayo huruhusu/huchochea bakteria na fangasi kuvamia na kuzaliana kirahisi .Hivyo fangasi hasa Candida Albicans wanazaliana sana na kushambulia uke.

(v) Kutokuwiana kwa homoni za mwanamke. Hali hii inasababishwa na vyanzo vingi mfano uzito kupita kiasi, ujauzito, wakati wa hedhi, n.k

(vi) Uchafu wa mavazi na uchafu wa mwili hasa kwa mwanamke ambaye hajui jinsi ya kujisafisha katika via vyake vya uzazi ili kuondoa seli zilizokufa (dead cells).

 Itaendelea wiki ijayo.


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment