The House of Favourite Newspapers

Sabby Angel Adaiwa Kufichwa Kenya

Sabrina Omary ‘Sabby Angel’

MREMBO ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’, anadaiwa kufichwa nchini Kenya na mwanamuziki anayekimbiza kwenye gemu la Hip Hop nchini humo, Khaligraph Jones ‘Khaligraph’.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha karibu kutoka Kenya ambacho kinafanya kazi kwa karibu na Khaligraph, wawili hao wapo kwenye uhusiano na ‘root’ nyingi za Kenya za Sabby anakwenda kwa mshikaji huyo.

Mikito Nusunusu haikupenda kulazia damu hilo, liliamua kumsaka Sabby kwa njia ya WhatsApp ili kufungukia madai hayo, alipopatikana alifunguka kwamba;

“Jamani watu mbona wambea hivyo! Kiukweli mimi nipo Kenya na kwa sasa muziki wangu ninafanyia huku lakini kuwa na uhusiano ha Khali, si kweli. Nina mtu wangu huku nninayefanya naye kazi lakini si yeye.”

Alipobanwa kuhusu kumtaja huyo mtu wake anayedai kuwa kwenye uhusiano naye alisema, hawezi kufanya hivyo kwani anaogopa kuibiwa na mastaa wenzake wa Kibongo.

Comments are closed.