The House of Favourite Newspapers

SABBY ANGEL APIGWA NDOA YA 5

Sabrina Omary ‘Sabby Angel’.

BUYU raha yake uupate ukiwa wa moto kutoka jikoni na siyo ule uliokaa juani ambao haunogi ukiumun’gunya! Ubuyu uliopo mezani wiki hii unaomung’unywa unamgusa mwigizaji ambaye anafanya vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’.

Sabby mwenye umri chini ya miaka 30, anadaiwa kupigwa ndoa ya 5 kwa siri kubwa ili mwanaume aliyemuoa asijue kama alishaolewa zaidi ya mara moja.

UBUYU WAMWAGWA

Kwa mujibu wa msambaza ubuyu makini ambaye alihudhuria harusi hiyo iliyofanyika jijini Nairobi nchini Kenya hivi karibuni, shughuli hiyo ilikuwa ya watu wachache mno na ndugu wa Sabby walikuwa ni wawili tu.

“Mimi nilijikuta nipo kwenye harusi hiyo kwa kuwa kuna rafiki wa huyo mwanaume aliyemuoa ambaye ni mtu wangu. “Nilishangaa mno maana ninajua huko nyuma Sabby alishaolewa mara nne,” alisema mtu huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Baada ya Ijumaa Wikienda kunyetishiwa ubuyu huo lilianza kumtafuta Sabby kwa njia ya simu baada ya kupatiwa namba na chanzo hicho cha habari ambapo alipoulizwa alijibu kama ifutavyo;

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Sabby? Kuna ubuyu umepigiwa ndoa nyingine ya tano inakuwaje?

Sabby: Hakuna cha inakuwaje hapo maana kuolewa ni bahati ya mtu.

Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo unaweza kuolewa zaidi ya hapo?

Sabby: Ndiyo kwani tatizo liko wapi?

Ijumaa Wikienda: Nini sababu ya kuachana na wanaume wote wanaofunga ndoa na wewe?

Sabby: Wao mara nyingi wana shida, wanaficha makucha pindi wanapotaka kuoa, lakini ukikaa nao ndani unagundua vitu vingi.

ANAJUA YEYE NI WA TANO?

Ijumaa Wikienda: Huyu wa sasa aliyekuoa anajua kuwa ulishaingia kwenye ndoa mara nne na yeye ni wa tano?

Sabby: Kwa nini nitumie muda mwingi kumuelezea mtu? Akikaa na mimi mwisho wa siku atakuja kuona au kujua tu.

Ijumaa Wikienda: Mbona kuna tetesi kuwa mara nyingi unaoolewa nao wanakuwa na pesa ndiyo maana unakubali kirahisi?

Sabby: Hakuna kitu kama hicho kwani mapenzi hayaangalii hilo.

Ijumaa Wikienda: Sasa mwanaume uliyeolewa naye ni mtu wa huko Kenya?

Sabby: Hapana, ni wa huko Tanzania, huku alipita tu kwenye biashara zake.

SKENDO YA PICHA ZA UTUPU

Ijumaa Wikienda: Ila hapa kipindi cha kati ulikumbana na skendo ya kuvuja kwa picha zako za utupu na anayedaiwa kufanya hivyo ni aliyekuwa mpenzi wako, vipi unazungumziaje?

Sabby: Hayo mambo sasa hivi yapo ndani ya sheria hivyo sipaswi kuzungumzia chochote.

Ijumaa Wikienda: Watu wengi wanafahamu wewe ni mwigizaji mzuri, lakini kwa sasa umepotea kwenye filamu, nini tatizo?

Sabby: Nimeona hailipi, nikahisi ninapoteza muda wangu bila sababu.

Ijumaa Wikienda: Mara nyingi hupendi kutulia sehemu moja, sababu kubwa ni kitu gani kinakufanya uwe hivyo?Image result for SABBY ANGEL

Sabby: Unajua mtafutaji hachoki, nitahangaika hivyohivyo mpaka nione sehemu sahihi ya kutulia.

Ijumaa Wikienda: Vipi mtoto wako analelewa na nani kama wewe unakuwa hukai sehemu moja?

Sabby: Mtoto wangu hana shida kabisa analelewa vizuri mno na bibi yake.

Ijumaa Wikienda: Hivi mtoto anapoona baba tofauti mara kwa mara anakuchukuliaje?

Sabby: Sidhani kama kuna shida kwa sababu mtoto wangu hakai na mimi sana.

Ijumaa Wikienda: Basi poa asante kwa ushirikiano.

Sabby: Karibu.

Comments are closed.