The House of Favourite Newspapers

Sabby Angel chupuchupu atoe meno

0

sabby-2

Sabrina Omary ‘Sabby Angel’

Stori: Imelda Mtema

MSANII anayepanda kwa kasi kwenye tasnia ya filamu Bongo,  Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ hivi karibuni alikumbana na kisanga kikali baada ya kudondoka kwenye ‘ tiles’ na kusababisha mguu wake kuumia vibaya.

Akizungumza na Uwazi Showbiz,  Sabby alisema kuwa tukio hilo lilitokea wakati anatoka bafuni baada ya kuoga ambapo kwa bahati mbaya aliteleza na kuumia mguu.

“Namshukuru Mungu kwa jambo lililotokea maana ilikuwa niangukie mdomo, sijui ingekuwaje kama ningetoa meno, lakini nilijitahidi kujikwepesha jambo lililosababisha  kuukandamiza mguu wangu chini na kuusababishia matatizo,” alisema Sabby.

Leave A Reply