The House of Favourite Newspapers

Sabby kumpa figo mama yake

0

sabbiStaa wa Filamu ya Sio Riziki, Sabrina Omary ‘Sabby’.

Na Imelda Mtema

STAA wa Filamu ya Sio Riziki, Sabrina Omary ‘Sabby’ amesema kuwa yupo tayari kujitolea figo moja na kumpa mama yake ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu.

Sabby alisema, kwa sasa ameamua kukatisha masomo yake nchini Marekani na kuja Bongo kwa ajili ya kumuuguza mzazi wake huyo.

“Tatizo la figo kwa mama yangu ni la muda mrefu na limekuwa likinikosesha raha mno. Kwa sasa nimejitoa kama wakiniambia inahitajika mtu atoe figo niko tayari kumpatia,” alisema Sabby.

Leave A Reply